Inatupasa Tuwathamini Walimu!

Recovered_JPEG Digital Camera_11583
Ni muda mrefu sasa tangu tuanze kusikia malalamiko na vitisho vya migomo ya walimu inayosababishwa na madeni na malimbikizo ya mishahara yao.

Malalamiko hayo yamekuwa kama ‘kelele za chura’ ambazo hazimzuii ng’ombe kunywa maji kwani si leo wala jana tangu malalamiko hayo yaanze, lakini yanaonekana kutojaliwa na mwajiri wao ambaye ni serikali.
Inasikitisha walimu wanapodharauliwa huku Serikali hiyo hiyo ikiongeza jitihada za
kujenga shule kila kata.

Shule hizo zitahitaji walimu, Je ni walimu gani mnaowahitaji huku hamuwajali? Ni elimu gani tunayoitaka huku chanzo cha elimu bora tukikidharau?
Fani ya ualimu imekuwa ni ya kudharauliwa siyo na serikali tu bali na jamii kwa
ujumla na hii ni kwa sababu tu serikali haioneshi mshikamano wowote na walimu hao
wala kusikiliza malalamiko yao.

Hapo hapo wanafunzi wakifeli mitihani yao watu wa kwanza kuwalaumu ni walimu. Je walimu hao watafundisha bila kuwezeshwa?
Elimu bora itabaki kama ndoto kila siku katika maisha yetu kama hatutowajali walimu hawa. Kama serikali itaendelea kutotoa ushirikiano wowote basi wanafunzi ambao ndio serikali ya kesho itaathirika, Tutapata wapi viongozi bora? Walimu wawe ni watu wa kuthaminiwa.

Na Theodora Malata, Dar es Salaam

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

2 thoughts on “Inatupasa Tuwathamini Walimu!

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.