Wanafunzi Watumia Karatasi Kujisitiri Hedhi!

Baadhi-ya-wanafunzi-wa-Shule-ya-Msingi-Lwengera-Darajani-wakiwa-wakati-wa-mapumziko-702x336

WANAFUNZI wa kike wanalazimika kutumia vitambaa na karatasi kujistiri katika kipindi cha hedhi kutokana na kukosa taulo za kike.

Akizungumza katika maadhimisho ya juma la elimu kitaifa (Gawe), yaliyoandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMet), Mwalimu wa Afya Shule ya Msingi Ikolo, Yohane Watli, amesema wanafunzi wa kike waliopevuka wengi  wanatumia karatasi na vitambaa kutokana na kukosa taulo hizo.

Amesema amewafundisha namna ya kuzikunja karatasi hizo na kuchomeka, ili mtoto asichafuke.

Kama unavyoona huku ni kijijini na wazazi hawana uwezo wa kununua taulo za kike, kwa hiyo ninachofanya kwa wale wa darasa la sita na saba ambao wameshapevuka na familia haina uwezo nawafundisha namna ya kutumia karatasi na ikijaa wanaenda kuitupa na wengine wenye uwezo wanatumia vitambaa vya nguo kuu,” alisema Watli.

Pia amesema shule hiyo haina sehemu maalumu ya watoto wa kike kujistiri, hivyo hulazimika kutumia vyoo vya mchanganyiko ambavyo pia matundu hayatoshi.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ikolo, Elibariki Haule, amesema kwamba shule hiyo ina wanafunzi 581 kuanzia darasa la awali hadi la saba ambapo wanahitaji vyumba vya madarasa 13 huku vilivyopo ni saba.

Haule amesema shule ina walimu 10 huku mahitaji yakiwa 13 na matundu ya vyoo manne ambapo mahitaji yao ni manne.

Pamoja na hayo, amesema  shule hiyo inahitaji kisima cha maji, kwani kwa sasa yanapatikana umbali wa kilomita tatu.

Mwanafunzi wa darasa la saba, Amina Salum, amesema kutokana na familia kukosa uwezo amefundishwa kutumia kitambaa wakati wa hedhi.

Mwalimu ametufundisha kutumia karatasi, tunazitumia pia chooni hakuna maji,” almesema.

NA HAPPINESS MNALE, MKALAMA |  ON

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.