Je, Wajua Hatua za Ukuaji wa Mtoto zipo sawa na Ukuaji wa Mmea wa Alizeti?

Ili kufanikisha mkakati wa kutokomeza udumavu na upungufu wa damu nchini, kuna tabia kadha wa kadha ambazo zinashauriwa kuzingatiwa ambazo zimegawanyika katika vipindi vinne vya Ukuaji wa Mtoto ambavyo vimefananishwa na mmea wa Alizeti.

IMG_20180604_010126
Namna Ukuaji wa Mmea wa Alizeti unavyolandana na Ukuaji wa Mtoto katika Hatua Nne (4). – USAID Mwanzo Bora Nutrition Program.

Hatua ya Kwanza

Hii ni hatua ya mbegu, ambacho ni kipindi cha ujauzito kwa mama yaani tokea mimba inatunga hadi mama anajifungua (miezi tisa).

Mambo muhimu ambayo yanasisitizwa katika hatua hii ni kama yafuatavyo;

 • Mahudhurio ya Kliniki, mahudhurio ya kwanza katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza.
 • Matumizi ya vidonge vya kuongeza damu katika kipindi chote cha ujauzito.
 • kuongeza ulaji wa vyakula vyenye madini chuma kwa wingi.
 • Matumizi ya vidonge vya Malaria (SP) na vya minyoo kama inavyoshauriwa na wataalam wa afya.

Hatua ya Pili ni (Mche) miezi 6 ya kwanza tokea mtoto kuzaliwa.

Katika kipindi hiki mama anashauriwa kuzingatia mambo yafuatayo:

 • Kumwanzishia mtoto kunyonya maziwa ya mama ndani ya lisaa limoja tokea kuzaliwa.
 • Kuhakikisha mtoto ananyonya maziwa ya kwanza ya rangi ya njano.
 • Unyonyeshaji wa mtoto maziwa ya mama pekee ndani ya miezi sita bila kumchanganyia kitu chochote hata maji.

Hatua ya Tatu (Kipindi cha Tumba) miezi 7 hadi 12.

 • Kumuanzisha mtoto chakula cha nyongeza mtoto baada ya miezi sita.
 • Mtoto katika kipindi hiki anatakiwa kupewa uji mzito.
 • Kuwalisha watoto wa zaidi ya miezi 6 vyakula mchanganyiko vikiwemo vyakula vya asili ya wanyama, mbogamboga na matunda.
 • kuendeleza unyonyeshaji wa watoto.
 • Kuongeza kiasi cha chakula na idadi ya milo kwa mtoto.

Hatua ya Nne (4) Ua (Mwaka 1 hadi miaka 2).

 • Watoto walishwe chakula cha familia.
 • Watoto waongezewe idadi ya milo pamoja na asusa katikati ya milo mikuu.
COSITA - Mradi wa Lishe wa Mwanzo Bora.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.