Usawa wa Kijinsia katika Kufundisha na Kujifunza.

kijinsia

Usawa wa kijinsia: Kutoa fursa sawa kwa wasichana na wavulana. Katika utoaji wa elimu usawa kijinsia unahusu kuhakikisha kuwa wasichana na wavulana wanapewa fursa sawa kuandikishwa shule, kushiriki katika ujifunzaji, kupata vifaa vya kujifunzia, kuthaminiwa kama binadamu na fursa nyingine za kielimu.

Mwalimu anapaswa kuhakikisha kuwa kuna usawa wa kijinsia katika shughuli zote za
kufundisha na kujifunza darasani. Hii inahusisha ushiriki sawa katika ujifunzaji, fursa sawa ya kupata vifaa vya kujifunzia na kusimamia usawa na haki za binadamu kwa wavulana na wasichana darasani.
Mtoto: Ni mtu mwenye umri chini ya miaka 18. Ukatili wa watoto ni wa aina yoyote ambao mtu hufanyiwa kabla ya kutimiza umri wa miaka 18.
Kunyanyasa mtoto kingono: Ni kitendo cha kumrubuni mtu yeyote mwenye umri chini ya miaka 18 kwa kumpa pesa au kitu chochote ili ushiriki naye ngono.
Unyanyasaji upo katika namna mbili:
Unyanyasaji wa kihisia: Ni hali ya kumwita mtu majina mabaya, kumfanya mtu ajihisi hana faida yoyote au hali ya kuhisi kutelekezwa (angalia vitendo vya kujijali sehemu ya kwanza).
Unyanyasi wa kimwili: Ni kama kupiga vibao, kusukuma, kupiga ngumi, kupiga mateke, mjeledi, kutishia kwa bunduki au kisu. (Imetoka katika andiko la unyanyasaji juu ya watoto-VACS: (2009)).

@Taasisi ya Elimu Tanzania, 2016

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

One thought on “Usawa wa Kijinsia katika Kufundisha na Kujifunza.

  1. naomba mfano wa shairi la tawasifu

    2018-06-11 21:45 GMT+03:00 Walimu na Ualimu :

    > Sir Gunda posted: ” Usawa wa kijinsia: Kutoa fursa sawa kwa wasichana na > wavulana. Katika utoaji wa elimu usawa kijinsia unahusu kuhakikisha kuwa > wasichana na wavulana wanapewa fursa sawa kuandikishwa shule, kushiriki > katika ujifunzaji, kupata vifaa vya kujifunzia, kuthami” >

    Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.