TECHNOLOGY | Q & A

 1. What does WWW stands for?
  1. World Wide Web (WWW) is a global hypermedia system on Internet.  It can be described as wide-area hypermedia information retrieval initiative aiming to give universal access to a large universe of documents.
  2. To use WWW the user needs a browser (eg. Internet Explorer, Firefox) that are used to display complex graphics, animation and sound.

Mwl. Gunda | 2019

You Educate a Girl and You Change the World, Make Sanitary Pads more widely Available to School Girls.

As part of a Friends’ of Education Movement activities on Friday 07, 2018 before International Literacy Day, Saturday, September, 2018, I was happy to initiate a step forward program “Malkia” to ensure more sanitary pads are widely available in Korogwe Rural Schools’.

WhatsApp Image 2018-09-08 at 12.48.51

To commemorate this International Literacy Day 2018, there are a lot of reasons for this. If there’s a need for help in girls literacy, we have to think about their health and hygiene at school.

WhatsApp Image 2018-09-08 at 12.47.06

Each year September 8th marks UNESCO’s International Literacy day, raising awareness globally on the issues surrounding adult and child literacy.

The Malkia campaign aiming to keep girls in school, if a girl doesn’t have access to sanitary pads or a safe and clean place at school to change them, that becomes another reason to keep her home. She starts missing a few days (4 – 7) every month, she falls behind, and she may eventually drop out.

This project is important to health and development—not only for the girls but for their communities and countries.

International Literacy Day is a day to remind world leaders, influencers and the general public of the current status of adult literacy and learning.

We are happy to welcome you all and share some experiences you have;

Mussa Gunda | A Friend of Education

mussa.gunda@jiandae.org | +255 674 14 12 09

Usawa wa Kijinsia katika Kufundisha na Kujifunza.

kijinsia

Usawa wa kijinsia: Kutoa fursa sawa kwa wasichana na wavulana. Katika utoaji wa elimu usawa kijinsia unahusu kuhakikisha kuwa wasichana na wavulana wanapewa fursa sawa kuandikishwa shule, kushiriki katika ujifunzaji, kupata vifaa vya kujifunzia, kuthaminiwa kama binadamu na fursa nyingine za kielimu.

Mwalimu anapaswa kuhakikisha kuwa kuna usawa wa kijinsia katika shughuli zote za
kufundisha na kujifunza darasani. Hii inahusisha ushiriki sawa katika ujifunzaji, fursa sawa ya kupata vifaa vya kujifunzia na kusimamia usawa na haki za binadamu kwa wavulana na wasichana darasani.
Mtoto: Ni mtu mwenye umri chini ya miaka 18. Ukatili wa watoto ni wa aina yoyote ambao mtu hufanyiwa kabla ya kutimiza umri wa miaka 18.
Kunyanyasa mtoto kingono: Ni kitendo cha kumrubuni mtu yeyote mwenye umri chini ya miaka 18 kwa kumpa pesa au kitu chochote ili ushiriki naye ngono.
Unyanyasaji upo katika namna mbili:
Unyanyasaji wa kihisia: Ni hali ya kumwita mtu majina mabaya, kumfanya mtu ajihisi hana faida yoyote au hali ya kuhisi kutelekezwa (angalia vitendo vya kujijali sehemu ya kwanza).
Unyanyasi wa kimwili: Ni kama kupiga vibao, kusukuma, kupiga ngumi, kupiga mateke, mjeledi, kutishia kwa bunduki au kisu. (Imetoka katika andiko la unyanyasaji juu ya watoto-VACS: (2009)).

@Taasisi ya Elimu Tanzania, 2016

Umuhimu wa Mwalimu kufahamu Sheria

Recovered_JPEG Digital Camera_13182

Ili mwalimu aweze kutekeleza kwa ufanisi wajibu wake mbele ya umma anapaswa awe na sheria na miongozo ambayo itamsaidia kuelewa vyema utumishi wake kama mtumishi wa umma.

Kanuni za Mpango wa Utumishi wa Umma za mwaka 2005, zilizotolewa kwenye Gazeti la Serikali namba 331 la tarehe 28/10/2005 ambazo zinahusu watumishi wa umma wakiwemo na walimu zinaonesha nyaraka za sheria ambazo mtumishi wa umma anapaswa kuwa nazo.

Kanuni ya 31 (1) ya kanuni hizo inaorodhesha nyaraka hizo kuwa ni;

 1.  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, (sura ya 2 R.E. 2002)
 2. Sheria ya Utumishi wa Umma (sura ya 298 R.E. 2002)
 3. Sheria ya Huduma ya Mafao ya Kustaafu (sura ya 371 R.E. 2002
 4. Sheria ya Mafao ya Kustaafu ya Viongozi wa Kisiasa (sura ya 225 R.E.2002)
 5. Sheria ya Huduma ya Umma (chombo cha upatanishi)
 6. Sheria ya Uajiri na Uhusiano wa Kazi (sura ya 366)
 7. Sheria ya Wakala wa Serikali (sura ya 245 R.E. 2002)
 8. Sheria ya Utawala wa Mkoa (sura ya 97 R.E. 2002)
 9. Sheria ya Taasisi za Kazi (sura ya 300)
 10. Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003
 11. Kanuni za Maadili na Tabia za Watumishi wa umma,
 12.  Kanuni mbalimbali za maadili na mwenendo wa wataalamu
 13. Kanuni za Serikali kwa ajili ya huduma za Umma
 14. Kanuni za kuajiri wahudumu wa umma
 15. Kanuni za nidhamu ya wahudumu wa umma
 16. Kanuni ya usuluhishi na mapatano ya huduma ya umma
 17. Kanuni za kustaafu na kuachishwa kazi ya huduma ya umma
 18. Kanuni ya sera ya uongozi na uajiri wa huduma ya umma
 19. Sheria nyingine za nyaraka zinazohusika kwa ajili ya marejeo yanayohusika

Je! Unafahamu muelekeo wa Elimu yetu kupitia Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014?

Capture

Sera hii mpya  (bofya hapa kuipakua >::::> Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014) inaweka Dira ya elimu na mafunzo nchini kuwa ni;

Mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi, umahiri, uwezo na mitazamo chanya ili kuweza kuchangia katika kuleta maendeleo ya Taifa” na

Dhima yetu kuwa ni;

kuinua ubora wa elimu na mafunzo na kuweka mifumo na taratibu zitakazowezesha kupata idadi kubwa ya Watanzania walioelimika na wanaopenda kujielimisha zaidi ili waweze kuchangia katika kufikia malengo ya maendeleo ya Taifa letu”.

Ili kufanikisha utekelezaji wa Sera hii kwa ukamilifu, kunahitajika ushiriki wa wadau wote wa elimu na mafunzo katika ngazi zote, ikiwemo sekta binafsi, Asasi za Kiraia (AZAKI) na washirika wengine wa maendeleo.

OLE WAO! WALIMU WANAOSHIRIKI VITENDO VYA UDHALILISHAJI KWA WANAFUNZI.

Serikali imesema haitavumilia vitendo vya  udhalilishaji ambavyo vimekuwa vikijitokeza katika baadhi ya shule hapa nchini na kusisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukukuliwa kwa wale wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo.

Image result for ndalichako
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako mkoani Dodoma wakati akikabidhi tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa katika masomo yao ya kuhitimu darasa la saba, Kidato Cha Nne na kidato Cha Sita kwa shule za serikali na zisizokuwa za serikali.
Waziri Ndalichako amewataka wanafunzi nchini kote kusoma kwa bidii, kuwa na nidhamu pamoja na kuishi kwa kufuata maadili ya kitanzania na siyo kuiga maadili ya watu wa nje.
“Wakuu wa shule nchini kote nawaagiza kuhakikisha mnasimamia kwa weledi malezi ya wanafunzi, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha walimu mnakemea vitendo vya udhalilishaji ambavyo vimekuwa vikijitokeza katika shule hapa nchini. Suala hili nasema si la kufumbia macho na wale wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa,” amesema Waziri Ndalichako.
Waziri Ndalichako amewaeleza wanafunzi hao kuwa suala la kupata ushindi ni rahisi lakini kudumu katika ushindi si Kazi nyepesi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Binilith Mahenge amewapongeza wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao kitaifa ambapo amesema Silaha pekee ya ujenzi wa Taifa na rasilimali za Taifa ni Elimu, ambapo pia amewataka wanafunzi kudumisha nidhamu na maadili.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Uingereza katika maadhimisho hayo ya wiki ya Elimu Gertrude Mapunda amesema serikali ya Uingereza itaendelea kuisaidia Serikali ya Tanzania katika kuboresha sekta ya Elimu.

Imetolewa na:
kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
08/06/2018

Je, Wajua Hatua za Ukuaji wa Mtoto zipo sawa na Ukuaji wa Mmea wa Alizeti?

Ili kufanikisha mkakati wa kutokomeza udumavu na upungufu wa damu nchini, kuna tabia kadha wa kadha ambazo zinashauriwa kuzingatiwa ambazo zimegawanyika katika vipindi vinne vya Ukuaji wa Mtoto ambavyo vimefananishwa na mmea wa Alizeti.

IMG_20180604_010126
Namna Ukuaji wa Mmea wa Alizeti unavyolandana na Ukuaji wa Mtoto katika Hatua Nne (4). – USAID Mwanzo Bora Nutrition Program.

Hatua ya Kwanza

Hii ni hatua ya mbegu, ambacho ni kipindi cha ujauzito kwa mama yaani tokea mimba inatunga hadi mama anajifungua (miezi tisa).

Mambo muhimu ambayo yanasisitizwa katika hatua hii ni kama yafuatavyo;

 • Mahudhurio ya Kliniki, mahudhurio ya kwanza katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza.
 • Matumizi ya vidonge vya kuongeza damu katika kipindi chote cha ujauzito.
 • kuongeza ulaji wa vyakula vyenye madini chuma kwa wingi.
 • Matumizi ya vidonge vya Malaria (SP) na vya minyoo kama inavyoshauriwa na wataalam wa afya.

Hatua ya Pili ni (Mche) miezi 6 ya kwanza tokea mtoto kuzaliwa.

Katika kipindi hiki mama anashauriwa kuzingatia mambo yafuatayo:

 • Kumwanzishia mtoto kunyonya maziwa ya mama ndani ya lisaa limoja tokea kuzaliwa.
 • Kuhakikisha mtoto ananyonya maziwa ya kwanza ya rangi ya njano.
 • Unyonyeshaji wa mtoto maziwa ya mama pekee ndani ya miezi sita bila kumchanganyia kitu chochote hata maji.

Hatua ya Tatu (Kipindi cha Tumba) miezi 7 hadi 12.

 • Kumuanzisha mtoto chakula cha nyongeza mtoto baada ya miezi sita.
 • Mtoto katika kipindi hiki anatakiwa kupewa uji mzito.
 • Kuwalisha watoto wa zaidi ya miezi 6 vyakula mchanganyiko vikiwemo vyakula vya asili ya wanyama, mbogamboga na matunda.
 • kuendeleza unyonyeshaji wa watoto.
 • Kuongeza kiasi cha chakula na idadi ya milo kwa mtoto.

Hatua ya Nne (4) Ua (Mwaka 1 hadi miaka 2).

 • Watoto walishwe chakula cha familia.
 • Watoto waongezewe idadi ya milo pamoja na asusa katikati ya milo mikuu.
COSITA - Mradi wa Lishe wa Mwanzo Bora.

Wanafunzi Watumia Karatasi Kujisitiri Hedhi!

Baadhi-ya-wanafunzi-wa-Shule-ya-Msingi-Lwengera-Darajani-wakiwa-wakati-wa-mapumziko-702x336

WANAFUNZI wa kike wanalazimika kutumia vitambaa na karatasi kujistiri katika kipindi cha hedhi kutokana na kukosa taulo za kike.

Akizungumza katika maadhimisho ya juma la elimu kitaifa (Gawe), yaliyoandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMet), Mwalimu wa Afya Shule ya Msingi Ikolo, Yohane Watli, amesema wanafunzi wa kike waliopevuka wengi  wanatumia karatasi na vitambaa kutokana na kukosa taulo hizo.

Amesema amewafundisha namna ya kuzikunja karatasi hizo na kuchomeka, ili mtoto asichafuke.

Kama unavyoona huku ni kijijini na wazazi hawana uwezo wa kununua taulo za kike, kwa hiyo ninachofanya kwa wale wa darasa la sita na saba ambao wameshapevuka na familia haina uwezo nawafundisha namna ya kutumia karatasi na ikijaa wanaenda kuitupa na wengine wenye uwezo wanatumia vitambaa vya nguo kuu,” alisema Watli.

Pia amesema shule hiyo haina sehemu maalumu ya watoto wa kike kujistiri, hivyo hulazimika kutumia vyoo vya mchanganyiko ambavyo pia matundu hayatoshi.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ikolo, Elibariki Haule, amesema kwamba shule hiyo ina wanafunzi 581 kuanzia darasa la awali hadi la saba ambapo wanahitaji vyumba vya madarasa 13 huku vilivyopo ni saba.

Haule amesema shule ina walimu 10 huku mahitaji yakiwa 13 na matundu ya vyoo manne ambapo mahitaji yao ni manne.

Pamoja na hayo, amesema  shule hiyo inahitaji kisima cha maji, kwani kwa sasa yanapatikana umbali wa kilomita tatu.

Mwanafunzi wa darasa la saba, Amina Salum, amesema kutokana na familia kukosa uwezo amefundishwa kutumia kitambaa wakati wa hedhi.

Mwalimu ametufundisha kutumia karatasi, tunazitumia pia chooni hakuna maji,” almesema.

NA HAPPINESS MNALE, MKALAMA |  ON

JE, UNAFAHAMU TABIA NA MIENENDO YA KIMAADILI KATIKA UTUMISHI WA UMMA?

UTUMISHIIli Utumishi wa Umma uwe wenye ufanisi na wa kuheshimika, watumishi wanapaswa kuzifuata Kanuni za Maadili ya Utumishi pamoja na kuwa na tabia na mwenendo unaozingatia mambo yafuatayo:

 1. Kutoa Huduma Bora
 2. Utii kwa Serikali
 3. Bidii ya Kazi
 4. Kutoa Huduma Bila Upendeleo

 5. Kufanya Kazi kwa Uadilifu

 6. Kuwajibika kwa Umma

 7. Kuheshimu Sheria

 8. Matumizi sahihi ya Taarifa

Kanuni hizi zimetungwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa  Umma kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa katika kifungu cha 34 cha Sheria ya Utumishi wa Umma ya Mwaka 2002 pamoja na Kanuni ya 65 (1) ya Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003.

Dar es Salaam,
Tarehe 11 Januari, 2005

Inatupasa Tuwathamini Walimu!

Recovered_JPEG Digital Camera_11583
Ni muda mrefu sasa tangu tuanze kusikia malalamiko na vitisho vya migomo ya walimu inayosababishwa na madeni na malimbikizo ya mishahara yao.

Malalamiko hayo yamekuwa kama ‘kelele za chura’ ambazo hazimzuii ng’ombe kunywa maji kwani si leo wala jana tangu malalamiko hayo yaanze, lakini yanaonekana kutojaliwa na mwajiri wao ambaye ni serikali.
Inasikitisha walimu wanapodharauliwa huku Serikali hiyo hiyo ikiongeza jitihada za
kujenga shule kila kata.

Shule hizo zitahitaji walimu, Je ni walimu gani mnaowahitaji huku hamuwajali? Ni elimu gani tunayoitaka huku chanzo cha elimu bora tukikidharau?
Fani ya ualimu imekuwa ni ya kudharauliwa siyo na serikali tu bali na jamii kwa
ujumla na hii ni kwa sababu tu serikali haioneshi mshikamano wowote na walimu hao
wala kusikiliza malalamiko yao.

Hapo hapo wanafunzi wakifeli mitihani yao watu wa kwanza kuwalaumu ni walimu. Je walimu hao watafundisha bila kuwezeshwa?
Elimu bora itabaki kama ndoto kila siku katika maisha yetu kama hatutowajali walimu hawa. Kama serikali itaendelea kutotoa ushirikiano wowote basi wanafunzi ambao ndio serikali ya kesho itaathirika, Tutapata wapi viongozi bora? Walimu wawe ni watu wa kuthaminiwa.

Na Theodora Malata, Dar es Salaam

Harakati za Marafiki wa Elimu ni nini?

Harakati za Marafiki wa Elimu ni nini?

Ni Harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini.

Recovered_JPEG Digital Camera_13182

Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala
yanayohusu elimu kwa lengo la kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa
programu mbalimbali za maendeleo ya elimu.

Mpaka Kufikia mwaka huu 2018, Harakati hizi zimekuwa na wanachama takribani 41,000 kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania.

Sera na mipango mbalimbali ikiwemo Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na Mpango wa Maendeleo ya Sekondari (MMES) inasisitiza umuhimu wa ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake. Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini.

Harakati za Marafiki wa Elimu zinalenga kukuza ushiriki wa wananchi katika michakato mbalimbali ya kuboresha elimu na demokrasia. Madhumuni ya Harakati hizi ni kuwawezesha watanzania kuleta mabadiliko katika elimu.

Harakati za Marafiki wa Elimu pia zitakupa fursa ya kubadilishana mawazo na
uzoefu na watu wengine wanaojali elimu na demokrasia.

Nani anaweza kuwa Rafiki wa Elimu?

Mtu yeyote anaweza kuwa Rafiki wa Elimu! Hakuna masharti. Unaweza kuwa kijana au mzee, mwanamke au mwanaume, mwenye ulemavu au asiye na ulemavu, aliye nje au ndani ya shule.

Licha ya watu binafsi, vilevile tunakaribisha maombi kutoka kwa wanafunzi, wazazi pia na walimu wanashauriwa kujiunga.

Wanawake na wasichana wanakaribishwa kujiunga kwa wingi kwani ushiriki wao una umuhimu wa kipekee katika kusukuma gurudumu la maendeleo ukizingatia kundi hili kihistoria limeachwa pembeni katika ngazi mbalimbali za maamuzi kwa muda mrefu.

Kwa Habari zaidi Bofya hapa PDF-Harakati za marafiki wa Elimu! au Wasiliana nasi kwa SMS au WhatsApp 0674141209.

What is a Lesson Structure?

 

A lesson Structure

Recovered_JPEG Digital Camera_11085

Is a detailed step-by-step guide that outlines the teacher’s objectives for what the students will accomplish during the course of the lesson and how they will learn it.

To be effective, a lesson has to include clear, easy to follow instructions; it has to have a clear objective—what we want students to walk away having learned or understood; and it has to be engaging enough to keep students interested and participating throughout. To achieve these goals, a well-defined lesson structure is indispensable.

Lessons that are effectively structured do not attack the main topic immediately, but rather ease into it in a number of ways. They may:

 • lead with a quote related to the subject to jumpstart discussion,
 • begin with a short activity that brings lesson themes into focus,
 • begin with a brief ritual to ready the group for a specific type of instruction.

The essential keys, then, of effective lesson structure can be summed up as:

 • A well-defined learning objective,
 • User friendly directions for teachers,
 • Differentiated instructional methods,
 • Engaging, enjoyable activities, and
 • A processing guide to connect participants’ lesson experience to real world applications.

 

There is something wrong with our world

unnamed

There is something wrong with our world, something fundamentally and basically wrong. […] The great problem facing modern man is that, that the means by which we live have outdistanced the spiritual ends for which we live. So we find ourselves caught in a messed-up world. The problem is with man himself and man’s soul. We haven’t learned how to be just and honest and kind and true and loving. And that is the basis of our problem. – Martin Luther King, Jr.