So why does this matter? And why should you take action to stop it?

 

unnamed

So why does this matter? And why should you take action to stop it?

Because child marriage robs girls of the right to make decisions about their own lives. Child brides are more likely to:

 • Drop out of school
 • Experience violence
 • Live in poverty

Today, you can help empower girls to resist the harmful practice of child marriage.

One day, we will live in a world where all women and girls have the freedom to determine their own futures.

Hii ni Wiki ya Elimu: Je, ni changamoto zipi zinaikabili sekta ya elimu nchini?

Hii ni #WikiYaElimu inayoadhimishwa kila mwaka wiki ya mwisho ya mwezi wa nne baada ya Mkutano Mkuu wa pili wa kiulimwengu wa elimu uliofanyika Dakar Senegal mwaka 2000 na kaulimbiu katika ngazi ya kitaifa ni “Uwajibikaji kwa Lengo la Maendeleo Endelevu lengo namba Nne na Ushiriki wa Wananchi.

Maadhimisho haya kitaifa yanafanyika mkoani Mtwara. Je, ni changamoto zipi zinaikabili sekta ya elimu nchini?

485716_443275602381579_861049680_n

Tunapoelekea kutengeneza nchi ya viwanda sekta ya elimu bado ina changamoto nyingi.

Gazeti la Tanzania Daima 26/04/2017 linaripoti kuwa shule ya msingi Michiga B wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara iliyoanzishwa miaka 12 iliyopita ikiwa na wanafunzi 743 wanatumia madarasa mawili tu.

Wakati huo huo shule hiyo inauhaba wa matundu ya vyoo ambapo wanafunzi 743 wanatumia matundu sita tu ya vyoo wakati walimu hawana kabisa vyoo na hivyo kulazimika kwenda kwa majirani wanaoizunguka shule hiyo.

Ni hatua gani zinaweza kuchukuliwa ili kuweza kutatua changamoto hizi na nyingine nyingi zinazoikabili sekta ya elimu?

ASILIMIA 11 DARASA LA SABA NANYUMBU MBUMBUMBU

Ikiwa maadhimisho ya wiki ya elimu yakiendelea, 11% ya wanafunzi wa darasa la saba huko Nanyumbu Mtwara hawajui kusoma wala kuandika.

18157785_1287194214704038_5619169717073497807_n

Kwa mujibu wa ripoti iliyofanywa na Taasisi ya TWAWEZA kuhusu uwezo wa wanafunzi kujifunza, imeonyesha kuwa asilimia 11 ya wanafunzi wa darasa la saba katika Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara hawajui kusoma wala kuandika.

Nanyumbu ni ya mwisho kati ya Wilaya tisa za Mkoa huo katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba wa mwaka jana huku changamoto kubwa ikiwa ni uhaba wa madarasa, hali inayosababisha wanafunzi kusomea chini ya mti na kwenye vyumba vya madarasa ya nyasi.

Wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Wilayani humo, Ofisa Utafiti Mwandamizi wa TWAWEZA, Richard Temu, alisema utafiti huo ulifanyika katika vijiji 30 vya Wilaya hiyo na Kaya 600 zilihojiwa.

Temu alisema, utafiti huo uliowahusisha wanafunzi wenye umri kati ya miaka saba hadi 16, unaonyesha kuwa asilimia 65 ya wanafunzi wa Wilaya hiyo hawahudhurii darasani huku asilimia 50 ya wanafunzi wa darasa la saba wakiwa hawajui kusoma kiingereza.

Aliongeza kwa kusema kuwa katika utafiti huo, walibaini kuwa asilimia 26 ya walimu hawahudhurii shuleni hali inayoendelea kusababisha ufaulu wa wanafunzi hao kuwa mdogo.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Nanyumbu, Salum Palangyo alisema utafiti huo umewafungua macho na kwamba utatumika katika kufuatilia maendeleo ya elimu.

By Kwanza Tv

TANGAZO KUHUSU NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI NA STASHAHADA KWA VYUO VYA SERIKALI NA VISIVYO VYA SERIKALI KWA MWAKA WA MASOMO 2017/18

Moja ya mikakati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika kuandaa walimu ni kuhakikisha kuwa wanaojiungana  Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada ni wenye sifa stahiki.

ftyttyt

Kwa kuzingatia hilo, waombaji wa mafunzo haya ni  wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu katika mtihani wa kuhitimu Kidato cha NNE na SITA.

Aidha, kutokana na  upungufu mkubwa wa walimu wa Sayansi na Hisabati, kipaumbele katika udahili kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo haya.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatangaza nafasi za mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada kwa mwaka  wa masomo 2017/18.

Masomo yataanza mwezi Julai, 2017.

Maelekezo ya tangazo hili yanawahusu waombaji wa mafunzo  ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na Visivyo vya Serikali.

MWISHO WA KUWASILISHA MAOMBI NI TAREHE 15/06/2017.

Bofya Hapa kuona sifa, Vigezo na Maelezo ya Jumla kwa kila Kozi: Tangazo la Mafunzo ya Ualimu kwa Mwaka wa Masomo 2017-2018

Leo ni siku ya Kumbukumbu ya Kuzaliwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, 13 April 1922

17903799_1323599647716493_6238104162789786669_n

Leo ni siku ya Kumbukumbu ya Kuzaliwa Baba wa Taifa hili na Mmoja wa waasisi wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Alizaliwa 13 April 1922 kijijini Butiama, wilayani Musoma, mkoani Mara.

Baadhi ya Nukuu zake Muhimu alizowahi kuzitoa kwa manufaa ya Taifa ni kama vile;

“Mara hii tu mmetajirika kiasi hicho? Kama mmeweza kutajirika kiasi hicho katika muda mfupi, fanyeni basi wote tutajirike, kwa nini mtajirike peke yenu?!””

“Mimi nang’atuka, lakini naendelea kuamini bila CCM madhubuti nchi yetu itayumba”.

Tukiruhusu ardhi iuzwe kama kanzu, katika muda mchache, kutakuwa na kundi dogo la Waafrika wakiwa na ardhi na walio wengi watakuwa watwana.”

Serikali ikitawaliwa na rushwa haiwezi kukusanya kodi, itabakia kukimbizana na watu wadogo wadogo tu”.

Mimi nimekaa Ikulu miaka 21, kuna biashara gani pale Ikulu?

Kwa mtu mwaminifu kabisa, Ikulu ni mzigo, si mahali pa kukimbilia hata kidogo”.

Kiongozi atakayepokea rushwa, tukimkamata tutamfunga miaka miwili na atapigwa viboko 24; 12 akiingia na kumi nambili akitoka, aende akamwonyeshe mkewe.

Ni miaka 17 kuelekea 18 sasa tangu Mwalimu afariki dunia kwa Ugonjwa wa kansa ya damu mwaka 1999.

MUNGU ilaze Roho yake Mahali Pema peponi.
Amen.

By Pio

MARUFUKU SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KUKARIRISHA DARASA, KUHAMISHA AU KUFUKUZA WANAFUNZI KWA KIGEZO CHA KUTOFIKIA WASTANI WA UFAULU ULIOWEKWA NA SHULE.

Wizara imebaini kwamba BADO kuna baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari hususan zisizo za Serikali na hasa zinazomilikiwa na Mashirika ya Dini  ambazo zinaendelea kukaririsha, kuhamishia shule nyingine au kuwafukuza shule wanafunzi kwa kigezo cha kutofikia alama za ufaulu zilizowekwa na shule ambapo ni kinyume cha sheria.

dsc02326

Kufuatia kuwepo kwa baadhi ya shule zinazoendelea na utaratibu huu, Wizara inatoa maagizo yafuatayo kwa utekelezaji:-

 1. Shule zote zilizowataka wazazi/walezi kuwahamishia watoto wao shule nyingine kwa kigezo cha kutofikia wastani wa ufaulu wa shule husika zinaagizwa kufuata agizo hilo na kuendelea na wanafunzi hao bila masharti yoyote.
 2. Wazazi na Walezi wenye Wanafunzi waliorudishwa nyumbani kwa sababu zilizotajwa hapo juu, wahakikishe wanawarudisha watoto wao kwenye Shule walizokuwa wakisoma ili waendelee na masomo kama kawaida.
 3. Shule ziwe na utaratibu wa kuinua viwango vya taaluma kwa wanafunzi wenye ufaulu mdogo, na hivyo sio ruhusa kukaririsha darasa mwanafunzi kwa kigezo cha kutofikia wastani wa ufaulu uliowekwa na shule.  Ikitokea ni lazima kufanya hivyo taratibu zilizopo zifuatwe.
 4. Wathibiti Ubora wa Shule, Kanda na Wilaya, Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya wanaelekezwa kusimamia utekelezaji wa agizo hili katika maeneo yao.
 5. Shule yoyote itakayokiuka maagizo hayo itachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria zilizopo.

IMETOLEWA NA:

Nicolas J. Buretta

KAIMU KAMISHNA WA ELIMU

 

Ajira Mpya za Walimu 2017: Serikali yatoa Ajira kwa walimu 3,081.

Serikali imesema jumla ya walimu 3,081 wakiwemo walimu 7 wa shule ya Sekondari Omumwani Kagera, wameajiriwa, hivyo bado kuna nafasi ya walimu 1,048 kati ya nafasi 4,129 za walimu wa Sayansi na Hisabati zilizotolewa kibali cha ajira.

12932622_1097677810296212_7417020322414204039_n
Taarifa hiyo imetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene alipokuwa  akizungumza na Waandishi  Habari,ofsini kwake ambapo amewataka walimu wote walioajiriwa wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi kuanzia tarehe 18 hadi 25 mwezi huu.

Amesema walimu walioajiriwa  wamepangwa moja kwa moja na TAMISEMI katika halmashauri zote nchini ambazo zina upugufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati.

Simbachawene amesema kati ya walimu hao walioajairiwa walimu 1,537 ni wa Shahada  na walimu 1,544 ni wa Stashahada.

“Sehemu kubwa ya walimu wa Shahada wamepangwa  kwenye shule za kidato cha tano na sita na wachache kwenye shule za kidato cha kwanza hadi cha nne’’ alisema.

Simbachawene amekiri  kuwa kuna upungufu wa walimu 26,026 wa masomo Sayansi na Hisabati katika shule mbalimbali za sekondari nchini.

“Moja ya changamoto kubwa ambazo zinaikabili sekta ndogo ya elimu ya sekondari ni upungufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati upungufu uliopo  katika shule 3,602 ni 26,026 sawa na asilimia 60.14 ya walimu 43,248 wanaohitajika” amesema Simbachawene

Amesema walimu wanaohitajika kwa masomo hayo ni walimu 43,248 lakini waliopo kwa sasa ni 17,252 pekee.

Amesema kwa sasa serikali ina shule za sekondari 3,602 na kati ya hizo shule 333 ni za kidato cha tano na sita huku zingine 54 za kidato cha tano zimeanzishwa .

Aidha amesema shule hizo za sekondari kwa upande wa masomo ya Sanaa ina ziada ya walimu 7,463 ambapo waliopo ni walimu 63,240 na wanaohitajika ni walimu 55,777.

“Kutokana na ziada hiyo ya walimu wa Sanaa serikali imeanza kuchukua hatua yawahamisha walimu hao katika shule za msingi ili kuziba upungufu wa walimu katika shule hizo’’ alisema.

Bofya hapa kuona Majina: Orodha_ya_Walimu_wa_Ajira_Mpya_2017

Leo ni Kumbukumbu ya Kifo cha Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine – April 12 mwaka 1984!

17883690_1322394584503666_6278304343497397137_n

Leo ni siku ya Kumbukumbu ya Kifo cha Aliyekuwa waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine aliyefariki April 12 mwaka 1984 kwa Ajari ya Gari Dakawa – Morogoro,..na katika kuadhimisha siku hii ninakuleta baadhi ya Nukuu bora kabisa kutoka kwake.

“Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta: Kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote. Usalama wake ni kudra ya Mungu na Wananchi peke yake. Viongozi wazembe na wabadhirifu wahesabu siku zao. Labda tusiwajue. Hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo vyao viovu” – Sokoine, 26 Machi 1983

“Wajibu wa kila Mtanzania, kila familia na kila anayekula ni kujilisha mwenyewe. Si wajibu wa Taifa kumlisha mtu. Unaweza ukasaidiwa unapopatikana na janga. Lakini kama hakuna janga ni wajibu wa kila mtu aweze kujitosheleza kwa chakula na atoe ziada kwa Taifa” – Sokoine, 4 Oktoba 1983

“Vijana leo wengi wana mali zaidi kuliko wazee waliofanya kazi miaka thelathini hadi arobaini. Lakini wanaitaka Serikali ndiyo iwaulize mali hiyo wameipata wapi. Hivi kwa nini mzazi asimuulize mwanae, ‘mali hii umeipata wapi?'” – Sokoine, 23 Oktoba 1983

MUNGU ailaze Mahali pema peponi Roho yake ..Amen.

By Pio

HAKUNA KIONGOZI YEYOTE ANAYEKOSA USINGIZI KWA WEWE KUKOSA AJIRA!

Wakati wetu wakati tunasoma tulikuwa tunasoma kwa kushindana sana ili tu upate grade nzuri na upate mkopo chuo kikuu na kimbilio letu kubwa lilikuwa ni kusomea udaktari na ukikosa sana ualimu na tulikuwa na uhakika wa  kupata ajira.

 

DSC08267

Ni miaka takribani kumi imepita tukiwa na mawazo hayo, lakini sasa mambo yamebadilika lakini watu hawataki kukubali kama mambo yamebadilika, bado wana matumaini ya kuwa hali itakuwa sawa kama miaka kumi iliyopita, leo nataka nikwambie kama unafikiri hivo basi UMEPOTEA.

Ni miaka miwili sasa wenye taaluma zile ambazo zilikuwa zikihitajika sana sasa si dili tena, na watu bado wanasubiri matamko mbalimbali ya viongozi labda watawazungumzia hata wao lakini nataka nikwambie hakuna kiongozi yeyote yule anayekosa usingizi kwa kukosa kwako ajira na wala hawana wasiwasi kwani wanasubiri tarehe za mwisho wa mwezi wapokee mishahara yao na maisha yaendelee.

Wengi ambao hatuna ajira tumebaki kulalamika tu mwisho wa siku tunarudi ndani kuangalia TV tu na unajiita msomi asiyeweza hata kuwaza nje ya ajira, nakuhakikishia itafika mahali nyumbani watakuchoka na wewe umebweteka ukisubiri kiongozi fulani akuonee huruma haitakuja kutokea hata siku moja.

Nakushauri kama uko katika kundi hilo;

1. Acha kuchagua kazi kama huna kazi,
Fanya kazi yoyote halali ilimradi unaingiza hata sh.1 itakuwa na kuwa kubwa na hatimaye utaajiri wengine.

2. Fanya kazi za kujitolea.
Omba kazi ujitolee bure kwani saivi hamna mwenye shida na wewe, jitolee kwa dhati utaweza kumshawishi bosi wako akupe kazi.

3. Acha kujifanya msomi na wakati huna impact katika jamii.
Wakati wenzio wako wanachakalika na biashara ndogo ndogo wewe unaleta dharau na kudharau kazi zao, hizo dharau zitakuponza na utaendelea kulalamika mpaka mwisho.

4. Jishughulishe na kitu chochote si lazima kile ulichosomea.
Wakati watu wakiendelea kumaliza vyuo na kulundikana mtaani wakisubiri ajira wewe anza na kitu kidogo kikuze kidogokidogo na mwisho wa siku utashangaa una maendeleo makubwa na hutawaza tena ajira.

Anza sasa hujachelewa, mtaji wa kwanza ni akili yako na nguvu zako, sio lazima uanze na mamilioni ya pesa kuanzisha biashara.

“It doesn’t need money to make money”

Asante.

PIUS J. MULIRIYE@2017

UTARATIBU WA UHAMISHO KWA WATUMISHI WA UMMA

Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Sema ukweli hata kama unauma

1. Mamlaka za Uhamisho

Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na 8. ya mwaka 2002 ikisomwa na Kanuni zake pamoja na Taratibu za Uendeshaji za mwaka 2003 Mamlaka ya Uhamisho kwa watumishi wote wa Umma ni Katibu Mkuu Ofisi Ya Rais-Menejimenti ya Utumishi Wa Umma.

Kwa maelekezo ya Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi Wa Umma kwa barua Kumb Na. C/CB.271/431/01/62 ya tarehe 8/06/2006 na Kumb Na. C/CB.271/431/01/J/144 ya tarehe 27/08/2007 Mamlaka ya Uhamisho katika Uhamisho wa watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa yamekasimiwa kwa;

 1. Katibu Mkuu Ofisi Ya Waziri Mkuu TAMISEMI kwa watumishi wanaohama kutoka Halmashauri moja kwenda nyingine nje ya Mkoa;
 2. Katibu Tawala Mkoa kwa uhamisho wa watumshi wanaotoka Halmashauri moja kwenda nyingine ndani ya Mkoa na;
 3. Mkurugenzi wa Halmashauri kwa watumishi wanatoka kituo kimoja kwenda kingine ndani ya Halmashauri.

2. Aina za Uhamisho

Kuna aina mbili za Uhamisho, nazo ni;

 1. Uhamisho wa Kuomba

Taratibu za Kuomba Nafasi:-

 1. Mtumishi atapaswa kuomba nafasi ya uhamisho kwa kuwasilisha maombi yake ya uhamisho kwa Mkurugenzi wa Halmashauri au Mamlaka anayotaka kuhamia kupitia kwa Wasimamizi wake wa kazi katika kituo chake cha kazi alichopo na Mkurugenzi wake.
 2. Wasimamizi wa mtumishi anayeomba uhamisho watapaswa kuhakikisha maombi ya mtumishi yanafika katika mamlaka husika yakiwa na maoni yao kuhusu maombi hayo na sio kuzuia maombi. Iwapo kutakuwa na sababu ya msingi ya kuzuia maombi mwajiri amjulishe mtumishi kwa kumrejesha katika miongozo iliyopo
 3. Iwapo Mwombaji hataridhika na maoni /sababu za mwajiri /Msimamizi wa kazi kukataa maombi yake mwombaji atawasilisha maombi yake kwa Katibu Tawala wa Mkoa kwa ushauri na kama hataridhia maombi yatawasilishwa kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI yakiwa na vielelezo muhimu kuthibitisha maombi hayo kukataliwa na Mkurugenzi na kueleza sababu za yeye kuomba uhamisho huo.
 4. Mkurugenzi/Msimamizi wa kazi atayeombwa nafasi ya kuhamia atapaswa kumjibu mtumishi kupitia kwa Mkurugenzi wake kwa barua akimweleza kupatikana kwa nafasi hiyo kumetokana na nini ikiwa ni pamoja na kutaja Check Namba za watumshi waliofariki au kuacha kazi.
 5. Iwapo mtumishi wa umma ataomba uhamisho kwa sababu za kumfuata mume au mke, kujiandaa kustaafu baada ya kukaa miaka kumi nje ya mkoa anaotarajia kustaafia na kukaa katika kituo kimoja kwa zaidi ya miaka mitano anaweza kufikiriwa kugharamiwa gharama za uhamisho hata kama ataomba uhamisho mwenyewe.
 6. Mtumishi anayeomba uhamisho atapaswa kuwasilisha maombi yake kwa Katibu Mkuu au Katibu Tawala Mkoa au Mkurugenzi akiambatanisha barua iliyomkubalia kuhamia katika kituo anachotaka kuhamia. Aidha ni muhimu amjulishe mwombaji iwapo atagharimiwa uhamisho au la kufuatia kupata nafasi hiyo

Angalizo:

Hairuhusiwi Mtumishi yeyote kutumia mtu mwingine isipokuwa yeye mwenyewe au Mwajiri wake kwa njia ya posta au Mkono kuwasilisha maombi yake ya uhamisho. Inashauriwa kutumia njia ya EMS au regista kwa urahisi wa ufuatiliaji.

Upatikanaji wa Majibu:-

 1. Watumshi wote walioomba uhamisho watapata majibu yao kwa barua kupitia kwa waajiri wao na sio vinginevyo.
 2. Aidha kwakuwa uhamisho huu ni wa wazi watumishi waliokubaliwa au kaukataliwa uhamisho watapata taarifa za awali kupitia Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI yaani http://www.pmoral.go.tz mapema mwezi Julai kwa maombi yatakayopokelewa kuanzia Januari hadi Juni na mapema mwezi Januari kwa maombi yatayopokelewa kuanzia mwezi Julai hadi Desemba kwa kuwa Ofisi yetu imejipanga kushughulikia masuala ya uhamisho mara mbili kwa mwaka ili kuepusha mwingiliano wa majukumu katika vituo vya kazi kwa mwaka.
 3. Mtumishi atakayekuwa na malalamiko kuhusu maombi yake ya uhamisho anashauriwa kuelekeza maombi yake kwa Mamlaka iliyomwamisha kupitia kwa mwajiri wake na msimamizi wa kazi akiambatisha maombi yake ya awali na vilelezo vingine muhimu kama sababu za kuomba uhamisho na ushahidi wa kufikisha barua yake kwa Mamlaka ya uhamisho.
 4. Malalamiko ya mtumishi aliyeomba uhamisho na hakupata majibu au hakuridhika na majibu aliyopatiwa malalamiko yake yatashughulikiwa ndani ya siku saba bila kujali muda wa uhamisho yaani June au Desemba.
 5. Baada ya mtumshi kupata majibu /barua ya uhamisho atapaswa kuripoti ndani ya siku kumi na nne tangu amekabidhiwa barua yake ya uhamisho vinginevyo atachulikuliwa ni mtoro kazini.
 • Uhamisho wa Kawaida
 • Uhamisho huu ni wa kawaida ambapo Mwajiri au Msimaimizi wa kazi anafanya uhamisho kwa sababu za kuboresha utendaji.

  Hata hivyo ili uhamisho huo ufanyike pia Mamlaka za uhamisho zinatakiwa kujiridhisha uwepo wa nafasi wazi katika Halmashauri anayohamishiwa mtumishi wa hakusababishi upungufu katika Sehemu mtumishi anakotoka au anakohamia.

  Uhamisho huu kwa kawaida unagharamiwa na Halmashauri inayompokea mtumishi na ile inayomruhusu kwa kumlipa gharama za kufunga mizigo kama ilivyoelezwa kwenye Kanuni L (8 na 13) ya Utumishi wa Umma ya Kudumu toleo la 2009 na marekebisho yake ya mwaka 2010 kwa wakati. hivyo ni muhimu Mamlaka za Uhamisho kijiridhisha na uwezo wa Halmashauri kugharamia uhamisho huo ili kuepuka kuzalisha madeni kwa Serikali

  Pamoja na utaratibu wa uhamisho kuwa ni uhamisho kufanyika mara mbili kwa mwaka, uhamisho huu wa kawaida unaweza kufanyika wakati wowote katika jitihada za kunusuru utendaji katika kituo alichopo mtumishi au anachohamishiwa mtumishi kwa manufaa ya umma.

  Angalizo:

  Mtumishi atakayebainika kughushi saini za viongozi, kuomba au kupokea rushwa katika ngazi yoyote atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kumfikishwa mbele ya vyombo vya dola kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

  Ni muhimu kwa Waajiri kujiridhisha na majibu ya barua za uhamisho kutoka katika Mamlaka za uhamisho ili kuona kama maombi yake yalifuata taratibu sahihi na watumishi waliopata majibu wanatayarishiwa mapema data sheet na kumbukumbu za utumishi na mshahara ili kuepusha usumbufu kwa watumishi na waajiri wanaowapokea watumshi.

  Apply today for International Youth Camp Project – UVIKIUTA Tanzania (Chamazi Mbagala)

  Dear friends!

  We would like to share with you Youth camps opportunities available. We are looking for young men and women form the age of 16-30 to participate in these projects.

  Youth camps involve individuals and groups of youth who volunteer and live together on a project identified by a local community or a project working with that community.

  uvikiuta

  This is a personal-building experience, a journey not only through the geography of our planet, but also a Journey through the several cultures of our world, a self-discovering journey.

  The program aim at bringing together Youth from different cultures and backgrounds, promoting through practical actions, mutual understanding and lasting peace. It is a practical tool to demonstrate that living, working together and sharing knowledge is not only possible but rewarding.

  In the Youth camps we see the possibility of people to exchange experiences, learn more about other social, cultural, political and living conditions.

  Youth camps seek to provide an experience that connects service, culture, professional and personal growth. While the service we offer does improve the quality of life for others, it is equally important as a time to reflect on our own lives.

  The significance of what we do is more than social charity; it is an encounter with real people in the real world. Projects go beyond the familiar road of commercial society, taking us outside of our comfort zones so that we can spend our time in someone else’s shoes.

  By working with people in various cultures, we learn to recognize the world we all share.  We realize that our lives are interconnected and that our stories have common threads. Moreover by serving others we discover ourselves and better understand our own values and responsibilities as global citizen.

  Please find attached information, we are looking forward to receive application from you and your family members, friends and neighbors. Please do not keep this information. Share to your networks.

  Thank you,

  Ben Mongi

  Program Coordinator- UVIKIUTA

  Attachments;

  Download Project Information Sheet here: Youth Camps 2017

  Download Application Form Here: Youth Camps Application form

  Kumbukumbu ya Miaka 45 ya Kifo cha Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume

  Siku ya leo April 7, 2017 ni siku ya kumbukumbu ya miaka 45 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume ambaye alizaliwa mwaka 1905 na kufariki tarehe 7 Aprili 1972.

  Inaelezwa kwamba sababu za kifo chake kilitokana na kupigwa Risasi huko Kisiwandui Zanzibar alipokuwa akicheza bao na Marafiki zake.

  17800400_1315690075174117_3361023444776286517_n

  1905 – 1972

  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume

  Hayati Mzee Karume ambaye ni Mmoja wa Waasisi wa Taifa hili aliiongoza Zanzibar baada ya mapinduzi yaliyomwangusha Sultani aliyekuwa akitawala Zanzibar hadi mwanzoni mwa mwaka 1964.

   

  Na Baada ya miezi mitatu Zanzibar iliungana na Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na ndipo Muungano wa nchi hizi mbili ukazaa Tanzania.

  Mzee Karume alikuwa Makamu wa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  MUNGU ailaze Roho yake Mahali Pema Peponi.

  MUNGU ibariki TANZANIA

  Ni Jukumu letu sote kudumisha na Kuulinda Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar.

  @Sirgunda

  Ili kuimarisha Ulinzi na Usalama katika Taifa letu, hizi hapa ni namba za Makamanda wa Polisi Mikoa yote na Kanda zote Tanzania.

  17425817_10211714315308923_7914692761138490364_n

  Ili kuimarisha Ulinzi na Usalama katika Taifa letu, na kwasababu ni jukumu letu wananchi kuhakikisha tunaitunza amani yetu, hizi hapa ni namba za makamanda wa polisi mikoa yote na kanda zote Tanzania.

  Toa taarifa sahihi ya uvunjifu wa amani au viashiria vya uvunjifu wa amani, au mashaka na mtu au kundi la watu wenye kupanga uhalifu au mtu/watu wanaotafutwa na Jeshi la Polisi.

  RPC MWANZA 0715009949

  RPC MTWARA 0715009948

  RPC MOROGORO 0715009946

  RPC IRINGA 0715009921

  RPC SINGIDA 0715009959

  RPC TABORA 0715009961

  RPC KAGERA 0715009916

  RPC TANGA 0715009963

  RPC MBEYA 0715009931

  RPC RUVUMA 0715009956

  RPC DODOMA 0715009914

  RPC KIGOMA 0715009915

  RPC ARUSHA 0715009912/0754380176

  RPC MANYARA 0715009929

  RPC KINONDONI 0715009976

  RPC KANDA DAR 0715009983

  RPC NJOMBE 0658376495

  RPC SIMIYU 0658376481

  RPC ILALA 0715009980

  RPC TEMEKE 0715009979

  RPC GEITA 0658376488

  RPC SHINYANGA 0715009957

  RPC KASKAZIN UNGUJA 0715009918

  RPC KUSIN UNGUJA 0715009925

  RPC KUSINI PEMBA 0715009924

  RPCLINDI 0715009927

  RPC MARA 0715009930

  RPC TARIME LOLYA-RPC 0715009964

  RPC PWANI 0715009953

  RPC KILIMANJARO-0715009923

  RPC RUKWA 0715009954

  RPC Songwe 0677025491

  RPC Katavi 0658777778

  Kulinda Amani ya nchi ni Jukumu la Kila RAIA.

  Ajira Mpya za Walimu: Serikali haitamvumilia mwenye vyeti feki – Kairuki

  Inakadiliwa kuwa watumishi 4,300 wapya wanatarajiriwa kuajiriwa katika kada ya elimu na wasanifu wa maabara ambapo ajira hizo mpya zinakuja bada ya kukamilika kwa zoezi zima la kuhakiki watumishi hewa.

  Kairuki

  Hayo yamebainishwa mkoani Tabora na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma Mh. Angela Kairuki, wakati akizungumza na watumishi na wanachuo, ambapo amesema kuwa, kwa muda mwingi taifa limekuwa likikabiliwa na changamoto ya watumishi hewa huku likipoteza fedha nyingi.

  Aidha Mhe. Kairuki amesema kuwa kamwe serikali haitamvumilia mtumishi ambaye atabainika kuwa na vyeti feki, huku akiwataka watanzania kutambua madhara ya vyeti hivyo kuwa ni kutopatikana kwa huduma stahiki huku akiwataka wahitimu katika kada mbali mbali kutowaonea haya watu ambao wanataka kupora ajira za wenzao.

  Source@EATV.TV

  Ethical Hacker Boot Camp for 2017 – Tanga, Register NOW!

  Hacking

  Due to recent highly publicized hacks and high-profile data breaches, ethical hackers are in huge demand and being hired by almost every industry to help them keep their networks protected.

  So, it comes as no surprise that ethical hackers, penetration testers, and information security analysts are one of the most well-paid employees in the IT workforce today.

  There’s a growing number of jobs for people with ethical hacking skills. But if you lack behind in this field, you need a good computer hacking course to sharpen up your knowledge.

  And the good news for you is that this week’s Walimu na Ualimu Deals brings Ethical Hacking Boot Camp 2017 @ Tanga, that let you get started regardless of your experience level.

  The Ethical Hacking Boot Camp will walk you through the very basic skills you need to start your journey towards becoming a professional ethical hacker.

  How to Join This Boot Camp

  So, what you are waiting for? Call us 0674 14 12 09 grab the exclusive discounted deal NOW!

  Also stay tune for Course details next week Monday!

  @sirgunda