SIASA ZA UCHAGUZI 2010-2015

Imeandikwa na Nyanda Josiah Shuli
Imeandikwa na Nyanda Josiah Shuli

Naelekea kuchukia siasa zinazofanywa nchini kwetu. Kwa bahati mbaya sana zimekuwa ni siasa za uchaguzi tu. Aliyeko madarakani kazi yake ni kung’ang’ana asinyang’aywe tonge…aliye nje kazi yake ni kutaka kumwangusha aliyeko madarakani…siku moja yeye ndiye aaminiwe zaidi. Mitazamo yote hii miwili inatuletea siasa dhaifu sana. Leo hii wanasiasa wa vyama tofauti hawajui… na hawataki kufanya kazi kwa pamoja.

Hata katiba ambalo ni andiko la watanzania wote linataka kutekwa na wanasiasa…naelekea kuamini kwamba hata vyama mbadala wangepewa nafasi kuandika katiba mpya….ili tuichukue na kuipitisha bila maswali, nao wangeandika mambo yao tu. Wangejikita kwenye mambo yanayohusu taratibu za uchaguzi, muundo wa serikali na mambo ya tawala. Kimsingi hayo ndiyo baadhi ya mambo yaliyowafanya wadai katiba mpya.
Kila mwanasiasa angetambua kwambua kwamba Tanzania ni kubwa kuliko chama chochote kile, ni kubwa kuliko mtu yeyote yule. Sote tutapita na kwenda zetu…Tanzania itabaki. Ni Mungu mwenyewe ndiye ataendelea kuionabTanzania kila siku wakati ‘wachonga ngenga’ walishapita na wakapotea, watukanaji bungeni walishapita na kupotea, wadini walishapita na kupotea, nk…ila kwa bahati mbaya sana watakuwa wametuachia makovu ya kufumu-Mungu atuepushe na hili.
Bila wanasiasa wa itikadi tofauti kujua lini wapige siasa za uchaguzi na lini washirikiane kuleta maendeleo kwa watanzania na Tanzania tutakuwa kila siku tuko kwenye mashindano kama vile ya riadha. Fikiria mkimbiaji hodari Usian Bolt angekuwa anashindana kila siku, angeshachoka, angeshafulia, angeweza kushindwa na hata mtu dhaifu. Kwa nini wanasiasa wasiwe na mikakati ya kuhifadhi sehemu ya nguvu zao mpaka wakati muafaka ufike? Istoshe, kwa wale watakaofanya siasa za maendeleo watakuwa wamejiwekea mazingira mazuri baadaye.
Kila chama kinafanya siasa za uchaguzi toka 2010 mpaka 2015; mbaya zaidi siasa hizi zimeingia hadi ndani ya vyama hivi na kutengeneza makundi makubwa ambayo hayashirikiani kwa lolote. Ni mahasimu wa kisiasa. Hata uchaguzi wa 2015 ukiisha, zitaanza siasa za uchaguzi wa 2020.
Naanza kusadiki kwamba demokrasia ya kimagharibi imekuja mapema sana nchini kwetu. Wanasiasa, ambao ndio watawala wa sasa au watawala wa baadaye wameweka akili zao kwenye chaguzi, badala ya maendeleo. Mifano ipo mingi sana ya nchi ambazo tulilingana nazo kimaendeleo wakati tunapata uhuru-lakini wao wako mbali sana sasa. Kwa nini? Wao wanafanya siasa za uchaguzi-baadaye wanaelekea kwenye siasa za maendeleo mara chaguzi zinapoisha.
Kwa siasa zetu…hata tukibadili vyama katika utawala wa nchi tutaendelea kuvuna mabua. Wakenya wameshajua namna ya kushirikiana kama vyama. Lini washirikiane na lini waachane. Sisi kila siku tunaishia kuona kila linalofanywa na chama tofauti na tulichopo ni baya, halifai. Nimekosa imani na siasa za Tanzania. Nikiwa mtaalam wa mawasiliano nina mengi ya kuwashauri wanasiasa, ama vyama vya siasa-hasa namna ya kujenga mguso wa kudumu mioyoni mwa wananchi.
Mwl Nyerere alifanikiwa sana katika hili-bila kutumia makada waongo waongo, bila kutumia helkopta na bila kuwa na mitandao ya kushughulikia kambi tofauti au vyama tofauti. Kuna mbinu za kufanya hivyo-na hazina madhara wala kuhitaji bajeti kubwa. Niko tayari kuwashauri wenye nia ya kubadilika bila malipo.
Inakera sana kuona Bunge-tena la bajeti likiishia kwenye malumbano ya kiitikadi tu-huku likidonoadonoa bajeti kwa mbali-na propaganda zikichukua sehemu kubwa. Vyama vikuu CCM na CDM wamejielekeza huko. Nani atajadili bajeti? Labda TLP, UDP, NCCR na CUF. Je, peke yao wataweza? Istoshe nao wako kwenye ugonjwa ule ule wa siasa za uchaguzi…wa taifa au wa ndani ya vyama.
Poor Tanzania!

Wananchi tusiridhike na elimu isiyokuwa na tija

Nguvu muhimu ya kuchochea maendeleo katika jamii yeyote ni elimu bora. Elimu ambayo itawajaza wananchi maarifa tele, uwezo wa kufikiri, ujuzi wa mbinu mbalimbali za kutatua matatizo, ubunifu, ujasiri wa kuhoji, kudadisi, kujitambua na moyo wa uvumbuzi na fikra mpya zenye kutafsiri na kuzibadili changamoto kuwa fursa.

603887_519562718086200_1070368810_nElimu ya namna hii ndiyo inajenga daraja la maendeleo. Maana jamii kubwa ya watu itakuwa na uwezo wa kuzalisha na kushiriki moja kwa moja katika kujenga taifa lao.

Jitihada zetu za kujiletea maendeleo hazitaweza kufanikiwa iwapo elimu ya namna hii haipo katika jamii.

Na wananchi wakiwa wamelala bila kuhoji elimu yetu ya sasa inayotengeneza vyeti bandia na wasomi bandia hali itakuwa ngumu mno.

Wananchi kwa sasa tumeridhika na hali ya maisha. Hatufikirii vya kutosha  namna ya kuiboresha elimu yetu. Tumeridhika na vipimo dhaifu vya nini maana ya elimu na mazao yake katika jamii.  Lakini ukweli unasaliti kwa kuwa na wasomi wengi wasio na tija katika jamii.

Pamoja na kuelekeza jitihada zetu kwenye vitendea kazi kama vile majengo, madawati, sare za shule, vitabu, chaki, pesa na hata chakula na usafiri, yatupasa vilevile kuelekeza nguvu kwenye elimu; yaani nini mtoto anapata awapo shule. Hii ni kama vile mtoto ana maarifa gani, amefahamu nini baada ya kusoma, anaweza kufanya nini, anajiamini, anaweza kuthubutu, anaweza kuwasiliana vizuri, anajitambua, ni mbunifu, ni mvumbuzi, anajitihada za kufanyakazi, ni mjasiri na mwadilifu.

Hivyo, watanzania tuwe makini tutumie muda mwingi kukaa na watoto wetu na tuwapime ili kuhakikisha wanapata elimu kwa kutathimini viashiria vya elimu vilivyoainishwa. Na ndipo tutabaini ukweli wenyewe na kutafuta suluhisho la kudumu.

Tunajidanganya kuahirisha jukumu hili mihimu kwa kudhani kuna mtu atakuja kufanya badala yetu. Tumezifinya hata fikra zetu na kushindwa kufikiri sawa sawa kutokana na kunywa nadharia mfu za elimu bandia zinazothibitishwa na vipimo bandia.

Wananchi tuamke tufanye mapinduzi katika elimu.

Serikali imetelekeza vituo vya Walimu

Vituo vya walimu (TRCs) vilianzishwa hapa nchini miaka ya 1970. Hivi sasa kuna zaidi ya vituo vya walimu 600 nchi nzima. Baadhi ya malengo ya vituo hivi ni kuhamasisha walimu na wafanyakazi wa vituo vya walimu kuendeleza na kuinua taaluma zao kwa njia ya semina, warsha na mafunzo ya muda mfupi. Vilevile, kuwa sehemu ya kubadilishana uzoefu na taarifa kuhusu elimu.

Fedha nyingi inahitajika kuinua na kuhuisha vituo vya Walimu
Fedha nyingi inahitajika kuinua na kuhuisha vituo vya Walimu

Serikali imeshindwa kuendelea kutoa mafunzo kwa walimu kwa kutumia vituo hivyo kwa sababu viko katika hali mbaya kutokana na kutotengewa bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ambayo imechakaa na kugeuka maskani ya wadudu na vile vinaofanya kazi havina vitendea kazi vya kutosha.

Ni jukumu la serikali kufufua vituo vya walimu kwa kuvitengea bajeti kwa ajili ya kujiendesha na kuboresha miundombinu.

Vituo hivyo ni msaada mkubwa kwa walimu kujiendeleza kitaaluma ili waweze kukabiliana na mabadiliko ya mitaala ambayo inabadilika kila mara na pia walimu kufahamu mambo mbalimbali katika kukabiliana na changamoto za maisha pia ni fursa nzuri kwa walimu walio vijijini kuweza kupata taarifa mbalimbali kuhusu elimu na kubaduilishana uzoefu katika kazi yao ya ualimu.

MWONGOZO WA MBINU ZA KUFUNDISHIA SHULE ZA AWALI: SEHEMU YA PILI

Zana za Kufundishia

Kwa kuzingatia ufundishaji na hali halisi ya watoto wadogo, mwalimu anashauriwa kutumia ubunifu wake ili kupata vifaa vingi iwezekanavyo kwa kila aina ya vitendo. Mtoto anapaswa kuandaliwa na kutumia vifaa vinavyofaa kufundishia kila mada, kwa sababu hiyo mwalimu anashauriwa kutumia maarifa, stadi na uzoefu katika kuchagua mbinu na njia za kutumia kulingana na mazingira ya kijamii kutoka shule moja hadi nyingine.

Zana za Kufundishia na Kujifunzia
Zana za Kufundishia na Kujifunzia

Njia za Kufundishia na Kujifunzia

Mwalimu anashauriwa kuwahusisha watoto katika somo kwa njia za maelekezo, maswali mafupi pamoja na vitendo. Watoto watumie milango ya fahamu, kugusa, kuona, kusikia, kunusa na kuonja.

Hivyo kuna ulazima mwalimu kutumia vitu halisi, vifani, picha na vielelezo vingine katika kuwawezesha watoto kuelewa mada iliyo kusudiwa.

Tathmini ya Maendeleo na Uwezo wa Watoto

Kwa kawaida watoto wa darasa la awali hawapewi mitihani kama wapewavyo shule za msingi. Kutakuwa na upimaji wa maendeleo ya watoto kwa kuangalia uwezo wake. Kazi hii inafanywa kwa kuangalia kumbukumbu za maendeleo ya mtoto tangu alipoanza kuhudhuria shule ya awali hadi anapomaliza na kuandikishwa katika darasa la kwanza.

Ni muhimu mwalimu awe na utaratibu wa kuweka kumbukumbu zao.

Ubora wa Mwalimu

Ieleweke kuwa mwalimu ni nyenzo muhimu na kuu katika harakati za kufundisha na kujifunza. Ubora wa mwalimu kwa kiasi kikubwa unahusishwa na uwezo wake wa kumudu somo au mada anayofundisha. Aidha ufundishaji bora ni ule unaofanikisha na kuhusisha uchaguzi wa njia na mbinu sahihi za ufundishaji pamoja na vitendo vingi kufanywa na mwanafunzi badala ya mwalimu.

Maswali

 1. Taja madhumuni makuu manne (4) ya Elimu ya Awali.
 2. Taja sifa kuu nne (4) za Mwalimu wa Elimu ya Awali.
 3. Eleza kwa kifupi, Ubora wa Mwalimu ni upi?
 4. Taja mbinu mbalimbali zinazofaa kufundishia watoto wa shule ya awali.
 5. Taja vigezo vine (4) vinavyofaa kutumiwa na mwalimu wa Elimu ya Awali katika kuchagua mbinu na njia za kufundishia darasa lake.
 6. Nini maana ya zana za kufundishia na kujifunzia?
 7. Taja aina tatu (3) za zana za kufundishia na kujifunzia.
 8. Taja vitendo sita (6) vya masomo vinavyofundishwa katika shule za awali.
 9. Fafanua istilahi zifuatazo;
  1. Vitendo vya masomo
  2. Vitendo vya kujifunza
 10. Mazingira mazuri yanayovutia yanamsaidia mtoto kujisikia vizuri na kufurahia kuwepo shuleni. Mtot anapaswa awe huru na kuchunguza, kudadisi, kuuliza maswali na kujifunza. Ili mtoto apate uhuru huo mwalimu anapaswa kufanya mambo gani? Jadili.
 11. Kazi mradi (project) ni njia ya kufundishia ambayo huwafanya watoto wa elimu ya awali kujifunza kwa kushirikiana. Fafanua na toa mifano.
 12. Hakuna njia moja tu inayokidhi haja zote za kufundisha. Mwalimu fanisi ni Yule anayeweza kutumia njia zaidi ya moja wakati anapofundisha mada au somo. Fafanua.
 13. Eleza jinsi utakavyoweza kumsaidia;
  1. Mwanafunzi mwenye tabia ya utoro wa shule.
  2. Mwanafunzi anayeshindwa kujifunza.
  3. Mwanafunzi mwenye matatizo ya kuumwa mara kwa mara.
 14. Jadili, ni lini hasa unaweza kutambua kuwa mwanafunzi amepata maarifa, stadi na mwelekeo?
 15. Mtoto anajifunza kutokana na maarifa ya awali aliyonayo na jinsi anavyojihusisha na mazingira. Fafanua kauli hiyo.

MWONGOZO WA MBINU ZA KUFUNDISHIA SHULE ZA AWALI: SEHEMU YA KWANZA

Mwalimu wa Elimu ya Awali anapaswa awe na mvuto wa kutosha wa kupenda kufundisha shule ya awali.
Mwalimu wa Elimu ya Awali anapaswa awe na mvuto wa kutosha wa kupenda kufundisha shule ya awali.

Makala hii ni maalumu kwa walimu wa shule za awali. Kutambua na kuchagua Mbinu sahihi za kufundishia kwa mwalimu ni jambo muafaka katika kulea watoto.

Ikumbukwe kuwa ufundishaji wa watoto wa shule ya awali ni tofauti na ule wa shule za msingi. Mwalimu anatakiwa kuzingatia kuwa mtot wa umri huu katika shule ya awali hafundishwi masomo kama wale wa shule za msingi, badala yake watoto hawa hujifunza kwa vitendo, vonavyowapa msingi na kanuni mbalimbali za kuwakuza na kuwawezesha kukabiliana na maisha ya kawaida pamoja na kuwatayarisha kuanza elimu ya msingi.

Msisitizo mkubwa kwa mwalimu umewekwa katika matumizi ya mbinu shirikishi ambazo zitawawezesha watoto kushiriki katika kujadili, kuigiza kuwasiliana wao kwa wao, kufanya ziara na uchunguzi.

Mwalimu anatakiwa kubuni na kufaragua zana mbalimbali za kufundishia elimu ya awali. Aidha mwalimu bora wa elimu ya awali anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo;

 1. Awe na mvuto wa kutosha wa kupenda kufundisha shule ya awali.
 2. Ajiamini katika kushughulika na masuala ya elimu ya awali.
 3. Aweze kujiongoza na kuwaongoza wengine kama mtaalamu wa elimu ya awali.
 4. Ajifunze zaidi na kuthamini mawazo ya watu wengine ili kuboresha na kuendeleza shule ya awali.
 5. Apende na kuhimiza ushirikiano na mawasiliano na wadau wengine wa elimu ya awali.

Maswali:

 1. Eleza maana ya Elimu ya Awali
 2. Taja malengo matano (5) ya kufundisha na kujifunza malezi ya Elimu ya Aawali kwa Mwalimu daraja A.
 3. Eleza umuhimu wa Elimu ya Awali.
 4. Nini mtazamo wa Elimu ya Awali kwa jamii ya Tanzania?
 5. Kwa nini ongezeko la shule za awali ni kubwa mno maeneo ya mjini kuliko vijijini ambako kuna ongezeko la watu wengi?
 6. Taja aina kuu mbili (2) za uchunguzi wa mtoto wa Elimu ya Awali.
 7. Kuna aina anuai za kufanya uchunguzi wa mtot. Taja njia tatu (3).
 8. Taja njia nne (4) zinazoweza kueneza magonjwa ya watoto wadogo.
 9. Nchini Tanzania, Elimu ya Awali ilianza Mwaka gani?
 10. Ainisha aina kuu mbili (2) za uchunguzi wa mtoto na kila moja eleza kwa kutumia mifano miwili miwili kwa ufafanuzi.
 11. Watoto wadogo huwa na matatizo wakati wa kula. Je, matatizo hayo husababishwa na nini?
 12. Ni ajali zipi hutokea mara kwa mara katika Shule za Awali na husababishwa na nini?
 13. Taja na kueleza vifaa vinavyopaswa kuwemo katika Kisanduku cha Huduma ya Kwanza.
 14. Nini maana ya adhabu? Eleza faida na hasara za adhabu katika tendo la kujifunza.

Elimu Bora inazingatia nini hasa?

Elimu Bora ni ile inayozingatia masuala yafuatayo;

Elimu bora inazingatia Nini hasa
Elimu bora inazingatia Nini hasa

Hali ya Wanafunzi

Je, wako tayari na wanaweza kushiriki katika elimu yao? Je, wanapata ushirikiano kutoka kwenye familia na jamii zao?

Mazingira ya Kujifunzia

Je, ni salama kwa watoto wote bila kujali jinsia, imani na ulemavu? Je, vifaa kama vile madawati, vyoo na vitabu vinatosheleza mahitaji yote?

Mambo yanayofundishwa Darasani

Ni aina ipi ya ujuzi ambao Mitaala inatilia mkazo? Je, maudhui yake yanaendana na mahitaji ya jamii? Je, yanakuza uelewano, umoja, amani na haki za binadamu?

Walimu na Ufundishaji

Je, kuna walimu wa kutosha na wako tayari kufundisha? Je, ufundishaji unamjali mwanafunzi, na mahuasiano kati ya wanafunzi na mwalimu darasani yakoje?

Matokeo ya Elimu

Wahitimu wana aina gani ya maarifa, ujuzi na mtazamo? Na wanayatumiaje katika maisha yao ndani ya jamii?

Kuelekea Elimu Bora…..Ni nini kinafanyika darasani?

485716_443275602381579_861049680_n
Wadau mbalimbali tuna amini kwamba elimu bora inapaswa kuelekezwa kwenye stadi na ujuzi wa wanafunzi. Ili kufanikisha matokeo hayo muhimu, tunahitaji vitendea kazi-madarasa, walimu, vitabu vya kiada, maktaba, maabara na mazingira safi na salama.

Ili kuhakikisha watoto wanapata elimu bora, tunahitaji kujiuliza wenyewe;

Ni nini kinafanyika darasani? Walimu na wanafunzi wanafanya nini kufanikisha kujifunza? Ni jinsi gani wanatumia vitabu vya kiada, maktaba na maabara? Je, kila kitu kimepangiliwa kwa ajili ya watoto wetu kujifunza stadi wanazohitaji baadaye?

Wakati muafaka wa kuhamia kwenye elimu bora ni huu.

Tengeneza mitaala inayokubalika

Program ya elimu ni lazima ielekezwe kuendeleza stadi za watoto wanaohitaji kufanikiwa katika jamii.

Boresha mafunzo ya walimu

Walimu wanapaswa kulielewa vyema somo wanalofundisha. Wanapaswa kuwa msaada muhimu kuwapa hamasa wanafunzi katika somo na kuyafurahia masomo.

Upimaji halisi

Mtihani mmoja usiamue hatma ya baadaye ya watoto. Tunahitaji njia mbalimbali za kupima maarifa na stadi za watoto.

Honey, I’d rather you didn’t call….

Agree with your partner about the best time to call each other, especially in the office.

We all know that communication is necessary in every relationship. Besides face to face communication, the other most common mode is through telephone, to be specific, the mobile phone. It is a valuable too you need to talk to each other but are miles apart. The telephone is important, yes, but it can also cause a rift in your relationship, especially when misused.

It is important for every person in a relationship and we are also talking about marriage here, to be sensitive about when and how often to call their significant other because using the telephone carelessly could brew trouble for the two partners.

Calling at work

It is romantic to call your partner at work, “just because”. It tells them that you are missing them. However sweet your intentions might be, some careers or jobs do not allow employees to take “just because” calls.

A sensitive person will take the initiative to find out just how demanding his or her partner’s job is; otherwise the call will be a nuisance. Better still, find out the best time to call or send a text message.

When your call goes unanswered

When a call goes unanswered, most people’s reaction is to hit the roof, convinced that he or she has deliberately ignored your call. He could be in a meeting or it may simply not be the right time to call, do not insist on calling back, again and again – it is annoying.

When he finally calls back, your first question should not be, “why didn’t you pick my call?” accusations only make one defensive, and will get your blood pressure up for nothing.

Be cordial and pleasant, and if you must, ask him or her why your phone call went unanswered much later. If you’re one of those people tempted to make repeated phone calls to your partner, maybe it’s time you ask yourself whether you’re busy enough.

Some things to remember

Avoid calling during working hours unless it is absolutely necessary. Some employers frown on their employees spending too much time on the telephone, especially if their work does not just a lot of phone time. One of the ways out would be to agree with your spouse on the time to call each other, such as over lunch hour.

It is also good manners to call when you say s that you will call. It inspires trust and says that you are committed to the relationship and that you are a man, or woman, of your world.

Hali halisi ya Ualimu : Jukumu letu sote Kutimiza Wajibu

Ualimu ni nyanja muhimu katika Taifa lolote kwa mustakabali wa ubora wa Elimu kwa wananchi, maendeleo katika jamii na ukuaji wa uchumi. Wataalamu wengi  nchini katika sekta mbalimbali wanatokana na mwalimu. Mwalimu ndie aliyewajengea msingi mpaka kufikia hapo walipo.dsc002071.jpg

Lakini tukiangalia hali halisi ya walimu Tanzania ni duni kiasi cha kukatisha tama. Hali waliyonayo walimu wa Tanzania inafanya kazi ya ualimu kuwa ngumu na pia inawafanya watu wazidi kutoipenda.

Hali halisi inajionesha katika mazingira ya kufundishia, ukosefu wa vifaa vya kufundishia na idadi kubwa ya wanafunzi katika darasa lisilo na samani, mshahara mdogo wa walimu ambao hawapati kwa wakati, ukosefu wa mafunzo kazini ya kumwendeleza mwalimu na usambazaji duni wa walimu ambao hupendelea kufundisha shule za mijini kuliko vijijini.

Matumaini, ujasiri na kujituma kwa walimu leo hii kumetoweka hali ambayo inajionesha katika ufundishaji madarasani. Mwalimu hana muda wa kutumia mbinu wala njia yeyote ile ya kumfanya mwananfunzi ajifunze.

Kazi imebakia ni kumwelekeza mwanafunzi namna ya kujibu maswali ili afaulu mitihani bila kujali anaelewa anachojifunza au laa. Hali inayopelekea kupata maajabu ya watoto kufika shule za sekondari bila kujua kusoma na kuandika ipasavyo.

Hali hii mpaka lini, walimu tubadilike na tuone suala la kuwalea watoto na kuwapatia maarifa katika kujifunza ni jukumu letu kwani tukumbuke hata dini zetu zinatueleza kuwa tutakuja kuulizwa kwa kile tulichokifanya duniani basi iwe ni kwetu kujituma na kufanya kwa Baraka zetu na maslahi yaje kwa mustakabali mwingine. Tuwasaidie wanafunzi wetu kama wenetu.

Nasi wanafunzi tuwe chachu ya amani, furaha na faraja kwa walimu wetu ili wajione wanacho wanachojivunia licha ya hali halisi ilivyo kwani kwa kufanya hivyo ni moja ya kuibadilisha hali halisi na kupigania mapinduzi ya kweli ya haki zetu.

Wanajamii tuna kila sababu kuwa mstari wa mbele katika kuangalia elimu wanayopatiwa wanetu na tujiulize maswali kama kweli ndo tunachokihitaji kwa watoto wetu tunapowapeleka shule? Kama sicho basi itupelekee tupaze sauti zetu juu ya hali ya elimu nchini mwetu, tutoe mapendekezo na tushiriki katika kusaidia uboreshwaji wa elimu kwa ajili ya vizazi vyetu na vya wanetu.

Na kama wewe ni miongoni mwa watunga sera au una mamlaka ambayo yanaweza kupelekea kubadili hali hii ya elimu nchini mwetu basi tafakari na sikiliza vilio vya walimu, wanafunzi na wanajamii  iwe ni jukumu lako kuchukua hatua na kubadili hali halisi ili kuleta ufanisi na maendeleo nchini mwetu.

……..kila kitu kinawezekana sote ni chachu ya mabadiliko kufikia maendeleo endelevu ya kweli katika elimu.

Web 2.0 training opportunit​y

Hello ladies,

catKINU in collaboration with CTA will be hosting a 5-day Web 2.0 Learning Opportunity on 06 – 10 May, 2013. Participants will be introduced to selected web 2.0 applications including social media and will learn how to use them hands-on.

The Learning Opportunity will cover advanced online searching, getting information served via alerts and RSS, collaborating remotely using wikis and Google Docs, using VoIP, online mapping and social networking. Participants will get a chance to see what others have done, get hands-on experience on how to use innovative applications, and assess how they could adopt these innovations within the context of their work and organisation.

Applicants must be actively engaged in agriculture and rural development / natural resource management / biodiversity conservation in the domains of ICT for development (ICT4D), policies, markets; publishing, communication and media; and residents of Tanzania.

I have attached the flyer or Click Here to Read More…. 

If you have any questions please don’t hesitate to get in touch with me.

Also, please note, we will be hosting Girls Night Out this month at KINU, and the topic is Careers in ICT.

Regards,
Catherinerose
Co-Founder KINU

TUNYAMAZE?

 603887_519562718086200_1070368810_nWadau wa elimu wamesema mengi. Laiti wangesikilizwa, hali ya elimu nchini isingefika hapa ilipo. Kwa bahati mbaya sana, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi haikutoa nafasi kwa mawazo ambayo hayatokani na wao wenyewe, au watu ama taasisi wanazozichagua kuzisikiliza.

Usipoziba ufa, utajenga ukuta. Hatimaye Tanzania tumeanza kujenga ukuta. Tungeweza kuziba nyufa mapema-kuliko sasa tunapolazimika kujenga ukuta.

Sio kutokana na matokeo mabaya tu; ufundishaji na ujifunzaji umeshuka sana katika shule zetu na hali ya elimu nchini inazidi kuwa mbaya; hasa kuanzia elimu ya awali na ya msingi.

Hebu sasa mdau sema angalau jambo moja muhimu ambalo TUME YA MH. PINDA; au serikali kupitia wizara ya elimu wanapaswa kulizingatia.

Wana-HakiElimu tumeanzisha kampeni hii ya kukusanya jumbe fupi fupi za wadau kwa picha; au kwa maandishi; ambazo tutazikusanya na kuzifikisha kwa wadau.

TUMA PICHA YENYE UJUMBE AU MAANDISHI MAFUPI SASA KWENDA hakielimumedia@gmail.com.

Vyanzo vya Maarifa Vinajulikana?

Moja ,Elimu ni chanzo cha kwanza cha maarifa kwa binadamu. Elimu ambayo ni mchakato rasmi au sio rasmi wa kujifunza ndio maarifa ya kila namna hupatikana. Mwalimu kama muwezeshaji wa kwanza, humjengea mtu ari ya kutaka kujifunza kila siku na kumpatia mbinu za kujifunza.

Katika mchakato huo wa kujifunza ndipo mwalimu kama huweza pia kuhamisha maarifa kwenda kwa wanafunzi na kumfundisha mwanafunzi jinsi ya kujifunza ili awe mpenda kujifunza siku zote. Maana elimu haina mwisho. Bila kuwa na walimu wenye sifa za ualimu, maarifa ambayo ndio elimu yenyewe inakuwa vigumu kupatikana au yanapatikana nusunusu.

Pili,Vitabu ni chanzo kingine cha maarifa. Kila aina maarifa takikana yamo ndani ya vitabu. Yameandikwa tangu enzi za mababu zetu. Mathalani kwa waumini wa dini Biblia na Quran ni vitabu vya siku nyingi vyenye maarifa ya hali ya juu ambayo kamwe hayapitwi na wakati.

Tatu, Maandiko ya wanafalsafa. Wako wana falsafa kama akina Socrate, Plato, Jean Jaques, Rossauau, Paul Freire wameandika kanuni mbalimbali zenye maarifa tele ambazo hadi leo zinamsaidia binadamu kufanya maendeleo makubwa. Wapo pia akina Issack Newton ambao sidhani kama watakuja kusahaulika. Maandishi na vitabu vya hawa ni chanzo cha maarifa mengi kwa binadamu.

Pamoja na kuwa ukweli huu ni dhahri, je watanzania wangapi husoma vitabu? Maktaba nyingi zimefurika vitabu vyenye kila aina ya maarifa, lakini watu wengi hawana utamaduni wa kusoma vitabu.

Pata Habri kwa Urahisi
Pata Habri kwa Urahisi

Hata wasoni tunaotegemea huko vyuoni ni wachache wenye utamaduni wa kusoma vitabu. Wengi wanapenda njia za mkato.Je tutapaje maarifa kama hatuna utamaduni wa kusoma vitabu? Mwanafalsafa wa kimarekani John Khan aliwahi kusema ni bora ukose chakula kipindi Fulani lakini upate kitabu.

Ukweli huu aliutambua sana Mwalimu Nyerere ndio maana alikuwa msomaji mahiri wa vitabu. Pia alijua utakufa akaamua kuacha wingi wa maarifa kwa kuyaandika kwenye vitabu. Je hata vitabu vya Baba wa taifa tunavisoma? Au vipo kwenye makabati na mashelfu tu?

Nne, Vyombo vya habari.Inasemekana vyombo vya habari ni muhimili wanne wa dola/nchi yeyote. Kama hili ni kweli, basi umuhimu wa magazeti, Redio, Luninga, Intaneti na majarida ni mkubwa mno.

Vyombo vya habari ni chanzo cha maarifa. Kwa hiyo,tunapata maarifa mbalimbali, tunapata habari za matukio ya kila aina yanayotokea kila siku, tunapata taarifa kwa muda unaotakiwa na pia burudani. Tunapata mafunzo na maonyo yanayosaidia kumfanya binadamu makini ajiboreshe kila siku.

Taifa bila vyombo vya habari ni kama gari bila taa linasafiri usiku gizani. Tujiulize tena, Ni watanzania wangapi husoma magazeti? Ni watanzania wangapi husikiliza radio na kuangalia taarifa za habari na vipindi vingine kwenye luninga?

Ni kweli bado kuna jamii ambazo upatikanaji wa habari kwao ni tatizo kutokana na mazingira au umasikini.Lakini kwa watanzania wengi vyombo hivi vya habari vimesambaa hadi vijijini. Kwa sasa ni vigumu kukuta kijiji kizima hakuna Radio. Jamii kubwa inapata habari kupitia vyombo mbalimbali.

Pengine tatizo ni utashi wa wanajamii wenyewe kutafuta habari. Wapo watu wenyewe kutafuta habari.Wapo watu wasiopenda kabisa kusoma hata gazeti au kitabu. Tena hawa ni wengi hapa kwetu Tanzania. Mtu mwenye utamaduni wa kujisomea siku zote ana ari ya kutafuta habari.

Na huwa tofauti sana na mtu asiyejishugulisha kutafuta maarifa wala habari.Hata kama ni msomi wa namna gani ,kama ataridhika na usomi wake kisha akabweteka ,kamwe atabaki msomi wa cheti tu. Maana maarifa kila siku yanazaliwa mapya na hakuna mtu yeyote duniani anayejua yote.

Msomi wa shahada ya uzamivu (PhD) kwenye fani ya mawasiliano aliyeipata miaka ya 1980, nadhani hawezi kuwa mahiri wa teknolojia za sasa za mawasiliano japo ni msomi. Maana mambo mengi wakati anasoma hayakuwepo. Hivyo, bila kujishughulisha atabaki mbumbumbu kwenye eneo hilohilo alilopatia PhD, hadi asome tena ili ajue mapya.

Bila juhudi binafsi ni vigumu kupata maarifa au habari. Mfano unaweza kuwa na luninga lakini huiwashi, unaweza pia kuwa na gazeti lakini hulisomi. Hapa hakuna tofauti na yule ambae hana. Maana wanafalsafa husema kitabu usichokisoma ni sawa na hakipo!

Ni muhimu kujua kuwa binadamu hajegwi kama nyumba. Nyumba ndio hujengwa kuanzia msingi hadi kupaka rangi. Lakini binadamu hujijenga mwenyewe kwa juhudi binafsi za kujisomea na kutafuta habari. Hakuna mtu anayeweza kumjenga mwenzie muda wote. Hata walimu kazi zao kujifunza na kuonesha njia ili mwanafunzi ajenge utamaduni wakujisomea muda wote hadi uzeeni.

Hii inashabihi usemi usemao elimu ni bahari haina mwisho.Wingi wa maarifa ni utajiri wa leo na kesho. Bila maarifa huwezi kupata maendeleo.