Mbinu za Kufundishia

Mbinu na Njia za Kufundishia
Uchaguzi bora wa Mbinu na Njia za Kufundishia

Ni Jumla ya vitendo vya maandalizi ya somo linalokusudiwa, matumizi ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia, vitendo vya mwanafunzi katika harakati za kujifunza na jukumu la Mwalimu kinadharia na vitendo katika ufundishaji na ujifunzaji.

Maana ya Mbinu za Kufundishia

Ni mwongozo mbalimbali atumiao Mwalimu darasani wakati wa kuwasilisha somo alilioliandaa kwa wanafunzi wake.

Mwalimu anapashwa kuaamua kwa kuchagua kwa makini Njia na Mbinu bora za kufundishia ili wanafunzi wake waweze kujifunza kwa ufanisi.

Misingi ya kuchagua njia na mbinu ni kuzingatia mambo yafuatayo:-

Maudhui ya somo.

 • Mwalimu lazima azingatie hali ya somo, maarifa na stadi anayopaswa kujenga mwanafunzi.

Hali  na umri wa wanafunzi wako.

 • Mwalimu lazima azingatie umri wa wanafunzi, kukomaa au kutokomaa kwa akili za wanafunzi na mazingira yao ya nyumbani na ya shuleni.

Malengo ya somo.

 • Bainisha mambo ambayo wanafunzi wako wanataka kufanikisha katika maisha yao.

Uwezo wa Mwalimu juu ya somo au mada husika.

 • Zingatia uwezo wako, ujuzi, utaalamu ulionao katika kutumia mbinu au njia inayotarajiwa.

Vifaa na zana za kufundishia na kujifunzia.

 • Zingatia upatikanaji wa zana na vifaa shuleni au katika mazingira ya shule (Zingatia ufaraguzi wa Zana).

Vionjo na hali ya wanafunzi.

 • Njia au mbinu utakazotumia zioane na vionjo na hali za wanafunzi. Njia zisipingane na sifa hizo kwani malengo ya somo hayawezi kufikiwa.

68 thoughts on “Mbinu za Kufundishia

 1. kweli notic ni nzuri. nimezipenda
  Na ikiwa walimu wakitumia maudhui yake kwa ufasaha basi kiwango cha elimu kitaongezeka

  Like

 2. ni matini yenye mwongozo mzuri wa kuelewa dhana inayokusudiwa ila jitahidi kutokurudia misamiati katika maelezo mfano neno vionjo kwenye mstari wa mwisho nilitamani kuelewa vionjo ni nini ila nilishindwa kutokana na kuwa umerudia tena neno vionjo. ila hongera na nashukuru

  Like

 3. MASWALI HAYO PAMOJA NA BAADHI YA NUKUU YANATUWEZESHA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE KWA SABABU TUNAJIONGEZEA BAADHI YA UTAALAMU NA HATA MAARIFA KWA MASOMO YA UALIMU.TUTAFUTE NAMNA YA KUONGEZA UFANISI ZAIDI KATIKA ELIMU KWA AJILI YA KUKABILIANA NA SOKO LA AJIRA AFRIKAMASHARIKI.

  Like

 4. JINA:MAKINGI MARWA .MASWALI HAYO PAMOJA NA BAADHI YA NUKUU YANATUWEZESHA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE KWA SABABU TUNAJIONGEZEA BAADHI YA UTAALAMU NA HATA MAARIFA KWA MASOMO YA UALIMU.TUTAFUTE NAMNA YA KUONGEZA UFANISI ZAIDI KATIKA ELIMU KWA AJILI YA KUKABILIANA NA SOKO LA AJIRA AFRIKAMASHARIKI.

  Like

 5. Hongera kwa jitihada.Moja langu muali ni kwamba kila zama na kitabu chake.Ni vema mkaona katika zama hii ya TEHAMA,changamoto ya njia na mbinu tulirithishwa na kuzifanyia tafiti kama bado tunazihitaji.lakini pia ni vema kuzipendekeza si kuchezea tu maneno.Napendekeza njia na mbinu hizo ziitwe nyeti za kujifunza na kufundisha za zama zetu.

  Like

 6. Kwa mara ya kwanza najitokeza kwenye huu ukurasa nimependa namna mnavyoweza kufanya walimu wasihangaile kupata maarifa.
  Naomba mnisaidie tofauti kati ya mbinu na njia za kufundishia na kujifunzia.

  Like

 7. Pia katika suala zima La ufundishaji na ujifunzaji mwalimu anapaswa kutumia mbunu ya kuwatambua wanafunzi Wake tangu uwezo wao pia kujua na kufuatilia matatizo mbali mbali waliyo nayo wanafunzi Wake

  Like

 8. Kweli kabisa wadau tunatakiwa kuwa wabuifu ktk kuwasilisha mada na Somo fulan pia na mbinu shirikishi kwa Wanafunzi pia soma mazingira ubarikiwe sana

  Like

 9. Uko poa teacher mbinu imekaa vizurii saana nimeipenda pia ongeza mbinu na hata watoto watambue kufaragua zana

  Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.