Sheria ni nini?

make-d-world-a-beta-placemake-africa-d-sweetest-plc-to-b2.jpg
Kufanya Kilicho Sahihi

Sheria ni nini?

Sheria ni masharti yanayowekwa katika nchi ili kutoa mwongozo wa jinsi ya kufanya mambo kwa usahihi. Sheria lazima zifuatwe na watu wote, na anayevunja sheria huadhibiwa.

Kanuni ni nini?
Kanuni ni maagizo kwa ajili ya asasi kubwa ya umma, zinazoongoza kufanya mambo yaliyo sahihi. Kanuni hizi mara nyingi zinafafanua sheria za nchi.

Taratibu ni nini?
Taratibu ni maelekezo yanayotolewa kwa idara zote za serikali ili kuelekeza kufanya mambo yaliyo sahihi.

1. Mwalimu ni nani katika mazingira yetu ya Tanzania?
Neno “mwalimu” limetafsiriwa kwenye ‘Kamusi ya Kiswahili Sanifu’ TUKI (1981) kwenye ukurasa wa 201 kuwa ni “mtu afundishaye elimu au maarifa Fulani, au mtu anayeonesha wengine”.
Katika Sheria ya Elimu, (sura ya 353 R.E.2002), neon ‘mwalimu’ limepewa maana kwenye fungu la 2 (1) kuwa ni “mtu yeyote aliyesajiliwa kama mwalimu chini ya sheria hii.”
Na fungu la (46) la sheria hii, linaonesha kuwa baada ya mtu kusajiliwa na Kamishna wa Elimu na kupewa cheti, basi mtu huyo anakuwa mwalimu.

2. Umuhimu wa mwalimu kufahamu sheria
Ili mwalimu aweze kutekeleza kwa ufanisi wajibu wake mbele ya umma anapaswa awe na sheria na miongozo ambayo itamsaidia kuelewa vyema utumishi wake kama mtumishi wa umma.

Kanuni za Mpango wa Utumishi wa Umma za mwaka 2005, zilizotolewa kwenye Gazeti la Serikali namba 331 la tarehe 28/10/2005 ambazo zinahusu watumishi wa umma wakiwemo na walimu zinaonesha nyaraka za sheria ambazo mtumishi wa umma anapaswa kuwa nazo.

Kanuni ya 31 (1) ya kanuni hizo inaorodhesha nyaraka hizo kuwa ni;

 1.  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, (sura ya 2 R.E. 2002)
 2. Sheria ya Utumishi wa Umma (sura ya 298 R.E. 2002)
 3. Sheria ya Huduma ya Mafao ya Kustaafu (sura ya 371 R.E. 2002
 4. Sheria ya Mafao ya Kustaafu ya Viongozi wa Kisiasa (sura ya 225 R.E.2002)
 5. Sheria ya Huduma ya Umma (chombo cha upatanishi)
 6. Sheria ya Uajiri na Uhusiano wa Kazi (sura ya 366)
 7. Sheria ya Wakala wa Serikali (sura ya 245 R.E. 2002)
 8. Sheria ya Utawala wa Mkoa (sura ya 97 R.E. 2002)
 9. Sheria ya Taasisi za Kazi (sura ya 300)
 10. Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003
 11. Kanuni za Maadili na Tabia za Watumishi wa umma,
 12.  Kanuni mbalimbali za maadili na mwenendo wa wataalam
 13. Kanuni za Serikali kwa ajili ya huduma za Umma
 14. Kanuni za kuajiri wahudumu wa umma
 15. Kanuni za nidhamu ya wahudumu wa umma
 16. Kanuni ya usuluhishi na mapatano ya huduma ya umma
 17. Kanuni za kustaafu na kuachishwa kazi ya huduma ya umma
 18. Kanuni ya sera ya uongozi na uajiri wa huduma ya umma
 19. Sheria nyingine za nyaraka zinazohusika kwa ajili ya marejeo yanayohusika

3. Je, mtumishi wa kawaida anaweza kuzipata wapi hizi sheria na nyaraka anazopaswa kuwa nazo mtumishi wa umma?

Kwa mujibu wa kanuni ya 31 (2) na (3) ya Kanuni za Mpango wa Utumishi wa Umma za mwaka 2005 zinaeleza kuwa, “Kila mwajiri atapaswa kuhakikisha upatikanaji na fursa ya kutumia nyaraka zote anazopaswa kuwa nazo mtumishi aliye chini yake”.

Endapo unahitaji ushauri zaidi kuhusu Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma tafadhali wasiliana na Ofisi ya Raisi, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Anuani:

Ofisi ya Rais,

Menejimenti ya Utumishi wa Umma,

S.L.P. 2483,

Dar es Salaam.

Tovuti: www.estabs.go.tz

Barua pepe: permsec@stabs.go.tz

Simu: 2118531/4

Fax: 2125299

33 thoughts on “Sheria ni nini?

 1. Kwa kweli nimefurahishwa sana nakutoa elimu hii ningependa iwendelevu katika nyanja zote za kisiasa kiimani na kiafya ili jamii yetu iweze kuelimika.

  Liked by 1 person

 2. Nimependa sana kwa kuweka sheria mbarimbari wazi kwa jamii hii inaonyesha wa kuwa inchi yetu inatujari wananchi wake.Ninaomba kama inawezekana mnitumie sheria za kazi na nyinginezo nyingi zinazo muhusu raiya wa Tanzania kuwa nazo kwenye email hii.Asanteni sana.

  Like

 3. watumishi wa.serikali walio wengi hizo nyaraka hatuzipati hata mkipata mnapewa kimoja katika taasisi kwa hiyo inakuwa ngumu kila mmoja kupitia .nyongeza nyaraka zinazo patikana kwa ulahisi Ni katiba lakini vitabu vya kanuni inakuwa ngumu aksanteni

  Like

 4. law;is the sytem of rules that country or community recognizes as regulating the action of its members and mat enforce by the imposition of penalties by Anderson mtaremwa laurent bukoba TZ tuzisime sheria jamani hasa societys,footballers,bisnessman and so on…….

  Like

 5. Nimependa lkn mbona tukiajiriwa hizi sheria hatupewi zinaonekana mtumishi anapopatikana na kosa? Naomba web ninayoweza kupata hizisheria au kama hutojali nipostie kwenye e-mail adress yangu ”mbarikiwe sana”

  Like

 6. Walimu wengi hawajui sheria ,kanuni na taratibu za kazi, hii nikutokana na waajiri kutokuwapa fursa ya kuwaelimisha juu ya haki zao kisheria, wengi wamekuwa wakijikuta wanakosa hakizao au wanawajibishwa kwakutojuaa sheria, nashaurii kuwe na utaratibu wa kutoa mafunzo makazini juu ya haki na wajibu wa mwalimu

  Like

 7. Nimependa sana ufafanuzi huu ningeomba msaada juu ya ufafanuzi zaidi tafsiri ya R.E. Ningeomba uendelee kutfafanulia vifungu vya sheria na kanuni

  Like

 8. Ni kweli sheria iko sawa lakini tu naomba tuerimishe watumishi wa makapuni ya watu binafisi kama vile makapuni ya ulizi pia nauliza kujua sheria ya hali zangu ktk makapuni ya ulinzi ni sheria ngani inayotumika kusajiri makapuni ya ulizi

  Like

 9. Naitwa Sir. Donard Bahati Wa S.L.P 610 GEITA; Nimhitimu Wa Mafunzo Ya Ualimu Grade 3A 2016…. “Binafsi Nimependa Sana Kwani Nimejifunza Mengi Mazuri,ambayo Kimsingi Yameniimarisha Katika Idara Yangu.Zaidi Naiomba Serikali Itusaidie kuzipata Sheria na Miongozo Hii kwa urahisi Aidha Kwa Kuwatumia Ma Afsa Elimu Mikoa Ili Angalau Kueneza Semina Kwa Walimu Kuhusu Umhim Wa Vitu Hivi.Vilevile Sheria na Miongozo hii Ingeongezwa Ktk Mihtasari Ya Somo La Ualimu Vyuoni Ili Uwemsingi Mzuri Kwa Wahitimu Wa Mafunzo Haya. Nawatakia Mazuri Tu!.Sir.Donard Bahati (GEITA)

  Like

  1. Sijajua utaratibu wa mwl akimaliza likizo bila malipo inakuwaje? Naomba utaratibu.kwa afisa anayejua hilo

   Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.