Umuhimu wa Mwalimu kufahamu Sheria

Recovered_JPEG Digital Camera_13182

Ili mwalimu aweze kutekeleza kwa ufanisi wajibu wake mbele ya umma anapaswa awe na sheria na miongozo ambayo itamsaidia kuelewa vyema utumishi wake kama mtumishi wa umma.

Kanuni za Mpango wa Utumishi wa Umma za mwaka 2005, zilizotolewa kwenye Gazeti la Serikali namba 331 la tarehe 28/10/2005 ambazo zinahusu watumishi wa umma wakiwemo na walimu zinaonesha nyaraka za sheria ambazo mtumishi wa umma anapaswa kuwa nazo.

Kanuni ya 31 (1) ya kanuni hizo inaorodhesha nyaraka hizo kuwa ni;

 1.  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, (sura ya 2 R.E. 2002)
 2. Sheria ya Utumishi wa Umma (sura ya 298 R.E. 2002)
 3. Sheria ya Huduma ya Mafao ya Kustaafu (sura ya 371 R.E. 2002
 4. Sheria ya Mafao ya Kustaafu ya Viongozi wa Kisiasa (sura ya 225 R.E.2002)
 5. Sheria ya Huduma ya Umma (chombo cha upatanishi)
 6. Sheria ya Uajiri na Uhusiano wa Kazi (sura ya 366)
 7. Sheria ya Wakala wa Serikali (sura ya 245 R.E. 2002)
 8. Sheria ya Utawala wa Mkoa (sura ya 97 R.E. 2002)
 9. Sheria ya Taasisi za Kazi (sura ya 300)
 10. Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003
 11. Kanuni za Maadili na Tabia za Watumishi wa umma,
 12.  Kanuni mbalimbali za maadili na mwenendo wa wataalamu
 13. Kanuni za Serikali kwa ajili ya huduma za Umma
 14. Kanuni za kuajiri wahudumu wa umma
 15. Kanuni za nidhamu ya wahudumu wa umma
 16. Kanuni ya usuluhishi na mapatano ya huduma ya umma
 17. Kanuni za kustaafu na kuachishwa kazi ya huduma ya umma
 18. Kanuni ya sera ya uongozi na uajiri wa huduma ya umma
 19. Sheria nyingine za nyaraka zinazohusika kwa ajili ya marejeo yanayohusika

Mitaala – Maswali ya Kujipima | Siku 5 Kabla Mtihani wa GATCE

 1. Eleza maana ya mitaala.
 2. Eleza maana ya chanzo cha mitaala.
 3. Taja masomo yanayofundishwa kwenye mitaala ya Elimu ya Awali.
 4. Eleza kwa nini mitaala ya Elimu ya Awali hutilia mkazo wa kujifunza kwa vitendo na siyo nadharia?
 5. Eleza kwa nini masomo ya Stadi za Kazi yanafundishwa katika shule za msingi?
 6. Jadili juu ya Bunge kushiriki kuidhinisha matumizi ya mitaala ya shule na vyuo vya ualimu nchini.
 7. Jadili juu ya tathimini ya mitaala.
 8. Fafanua usemi huu, “Mwalimu ni mkuza mitaala”.
 9. Mitaala haina budi kubadilika kadri jamii inavyobadilika. Eleza
 10. Eleza tofauti iliyoko kati ya mitaala rasmi na mitaala isiyo rasmi.
 11. Majaribio na mitihani humpima mwanafunzi na mwalimu pia. Toa maelezo kutegemea hoja hizo.
 12. Taja na eleza vyanzo muhimu vya mitaala.
 13. Kwa nini Mitaala haina budi kuwiana na malengo ya taifa ya kutoa elimu?
 14. Nani mtuamiaji wa zana za kujifunzia na kufundishia? Mwalimu au mwanafunzi?
 15. Fafanua milango ya fahamu ya ndani na ya nje.
 16. Eleza tofauti baina ya chati na bango.
 17. Kwa nini si vizuri kutumia picha ikiwa vitu halisi vinapatikana?
 18. Mambo gani yanayokufanya utumie ubao wa chaki darasani?
 19. Eleza kazi ya ubao wa vielelezo darasani.
 20. Eleza jinsi utakavyotumia picha au chati katika darasa lililojengwa kwa nyasi au makuti.
 21. “Ubao wa chaki ni kwa matumizi ya mwalimu na mwanafunzi” Jadili usemi huu.
 22. Eleza kwa kifupi njia zinazoweza kusaidia zana kudumu kwa muda mrefu zaidi
 23. Taja sifa 6 za chati na mabango mazuri.
 24. Taja zana mbili za kujifunzia/kufundishia ambazo ni lazima ziwepo wakati somo likiendelea.
 25. Nini maana ya zana za kufundishia?
 26. Eleza hatua nne ambazo unaweza kupitia kutengeneza ubao (wa chaki) huru.
 27. Ufaraguzi wa zana ni nini? Kwa nini tunafaragua zana?
 28. “Matumizi ya zana huchangamsha milango ya fahamu ya mwanafunzi”. Jadili usemi huu.
 29. Sifa zipi za chati au mabamngo zinapotumika darasani zinaweza kusababisha mwanafunzi kujifunza elimu potofu.
 30. Elimu ni nini?

Stadi za Kazi – Maswali ya Kujipima | Siku 5 Kabla Mtihani wa GATCE

 1. Taja faida za Elimu ya Michezo
 2. Taja vipengele vilivyomo katika muhtasari wa mafunzo ya Elimu kwa Michezo katika shule za msingi.
 3. Ni mavazi gani yanayofaa kwa mwanamichezo?
 4. Taja vifaa muhimu kwa mchezo wa netiboli.
 5. Chora uwanja wa mchezo wa wavu na kuonesha vipimo vyake.
 6. Kwa nini wachezaji hubadilishana wakati mchezo unapoendelea katika mchezo wa mpira wa kikapu?
 7. Taja kanuni kuu za kutoa huduma ya kwanza.
 8. Kambi ni nini? Taja vitu muhimu vya kuzingatia wakati unatayarisha kupiga kambi.
 9. Sanaa ni nini? Taja aina za sanaa.
 10. Mapambo ni nini?
 11. Kuna aina ngapi za tamthilia? Zitaje na toa maelezo kuhusu aina hizo.
 12. Eleza matukio ambayo hutumia muziki kama chombo cha kuvutia usikivu.
 13. Fafanua na chambua sifa tatu za michezo ukionesha umuhimu wake katika ukuaji wa mtoto;
  1. Kimwili
  2. Kiakili
 14. Kuna umuhimu gani kwa mwalimu wa michezo kufahamu huduma ya kwanza?
 15. Kuna sababu gani za msingi kwa mwanamichezo kupasha miwli joto kabla ya kuanza kucheza mchezo wowote?
 16. Muhtasari wa Michezo na sanaa kwa shule za msingi una vipengele vingapi?
 17. Taja sababu zilizofanya makabila mengi kuthamini na kuhusisha michezo na sanaa kwa watoto na vijana wao.
 18. Utazingatia taratibu zipi wakati unafanya maandalizi ya kufundisha somo la michezo kwa watoto wadogo (chekechea)?
 19. Eleza tofauti ziliyopo kati ya michezo ya awali na michezo ya sasa.
 20. “Michezo ni uhai” Jadili ukitoa mfano kutegemea jibu lako.
 21. Utatumia mbinu gani ili kuwafanya wanafunzi wako wapende kucheza michezo?
 22. Jadili misingi mitatu ya elimu ya jadi.
 23. Taja na eleza sababu tatu zilizofanya kipindi cha ujana kuwa na matatizo.
 24. Njia ya kualika wageni na njia ya ziara zinafanana katika matayarisho yake. Fafanua mambo yanayozifanya njia hizo zifanane na eleza faida mbili za kutumia njia hizo kwa pamoja.
 25. Kwa nini mwalimu analazimika kujenga tabia ya udadisi kwa wanafunzi wake? Toa sababu tano.
 26. Eleza jinsi mazingira yanavyoathiri maisha ya jamii ya siku kwa siku.
 27. Eleza jinsi utakavyofundisha somo la utamaduni kwa kutumia michezo.
 28. Taja vipengele vine vinavyoingizwa katika sanaa za ufundi.
 29. Eleza jinsi utakavyoishirikisha jamii inayozunguka shule yako katika kufundisha somo la utamaduni.
 30. Fafanua dosari zinazoweza kutokea katika ufundishaji iwapo mwalimu hakuandaa vyema Somo Lake.