Umuhimu wa Mwalimu kufahamu Sheria

Recovered_JPEG Digital Camera_13182

Ili mwalimu aweze kutekeleza kwa ufanisi wajibu wake mbele ya umma anapaswa awe na sheria na miongozo ambayo itamsaidia kuelewa vyema utumishi wake kama mtumishi wa umma.

Kanuni za Mpango wa Utumishi wa Umma za mwaka 2005, zilizotolewa kwenye Gazeti la Serikali namba 331 la tarehe 28/10/2005 ambazo zinahusu watumishi wa umma wakiwemo na walimu zinaonesha nyaraka za sheria ambazo mtumishi wa umma anapaswa kuwa nazo.

Kanuni ya 31 (1) ya kanuni hizo inaorodhesha nyaraka hizo kuwa ni;

 1.  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, (sura ya 2 R.E. 2002)
 2. Sheria ya Utumishi wa Umma (sura ya 298 R.E. 2002)
 3. Sheria ya Huduma ya Mafao ya Kustaafu (sura ya 371 R.E. 2002
 4. Sheria ya Mafao ya Kustaafu ya Viongozi wa Kisiasa (sura ya 225 R.E.2002)
 5. Sheria ya Huduma ya Umma (chombo cha upatanishi)
 6. Sheria ya Uajiri na Uhusiano wa Kazi (sura ya 366)
 7. Sheria ya Wakala wa Serikali (sura ya 245 R.E. 2002)
 8. Sheria ya Utawala wa Mkoa (sura ya 97 R.E. 2002)
 9. Sheria ya Taasisi za Kazi (sura ya 300)
 10. Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003
 11. Kanuni za Maadili na Tabia za Watumishi wa umma,
 12.  Kanuni mbalimbali za maadili na mwenendo wa wataalamu
 13. Kanuni za Serikali kwa ajili ya huduma za Umma
 14. Kanuni za kuajiri wahudumu wa umma
 15. Kanuni za nidhamu ya wahudumu wa umma
 16. Kanuni ya usuluhishi na mapatano ya huduma ya umma
 17. Kanuni za kustaafu na kuachishwa kazi ya huduma ya umma
 18. Kanuni ya sera ya uongozi na uajiri wa huduma ya umma
 19. Sheria nyingine za nyaraka zinazohusika kwa ajili ya marejeo yanayohusika

JE, UNAFAHAMU TABIA NA MIENENDO YA KIMAADILI KATIKA UTUMISHI WA UMMA?

UTUMISHIIli Utumishi wa Umma uwe wenye ufanisi na wa kuheshimika, watumishi wanapaswa kuzifuata Kanuni za Maadili ya Utumishi pamoja na kuwa na tabia na mwenendo unaozingatia mambo yafuatayo:

 1. Kutoa Huduma Bora
 2. Utii kwa Serikali
 3. Bidii ya Kazi
 4. Kutoa Huduma Bila Upendeleo

 5. Kufanya Kazi kwa Uadilifu

 6. Kuwajibika kwa Umma

 7. Kuheshimu Sheria

 8. Matumizi sahihi ya Taarifa

Kanuni hizi zimetungwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa  Umma kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa katika kifungu cha 34 cha Sheria ya Utumishi wa Umma ya Mwaka 2002 pamoja na Kanuni ya 65 (1) ya Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003.

Dar es Salaam,
Tarehe 11 Januari, 2005

Ikulu yatoa Waraka Mzito kwa Watumishi wa Umma Wanaotaka Kugombea Nyadhifa Mbalimbali za Kisiasa Nchini.

jkIkulu imetoa waraka mpya kwa watumishi wa umma wenye nia ya kuwania nafasi mbalimbali za kisiasa, ikiwamo urais, ubunge na udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

 Kwa mujibu wa waraka huo, mtumishi wa umma anayetaka kuwania moja ya nafasi hizo za kisiasa, atalazimika kuacha kazi na kulipwa mafao yake, endapo jina lake litateuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kama mgombea.
Waraka huo wenye Kumbukumbu CAB 157/547/01/47 ukiwa na kichwa cha habari ‘Kuhusu utaratibu kwa watumishi wa umma wanaogombea nyadhifa za kisiasa nchini’, umetolewa Januari 2, mwaka huu na kusainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
Pamoja na mambo mengine, utaratibu huo umelenga kuondoa upendeleo katika utoaji huduma kwa wananchi na matumizi mabaya ya ofisi kunakofanywa na baadhi ya watumishi wa umma wenye nafasi za kisiasa.
“Baadhi ya watumishi wa umma wenye nafasi za uongozi wa kisiasa wamekuwa wakitoa huduma kwa upendeleo, hususani pale anayehudumiwa akiwa mpigakura wake au anatoka katika chama chake cha siasa,” unasema waraka huo..
Waraka huo uneongeza kuwa baadhi ya watumishi hao wa umma wenye nafasi za kisiasa, wamekuwa wakitumia nafasi walizanazo katika ofisi zao kushawishi watumishi wenzao kupigia kura chama fulani au mgombea fulani.
Aidha unasema upo uwezekano wa kuwapo mgongano wa kimasilahi baina ya siasa na utumishi wa umma, ambao unaweza kusababisha baadhi ya watumishi wasio waadilifu kutoa siri za Serikali kwa masilahi ya kisiasa.
“Katika baadhi ya kazi imekuwapo migongano baina ya watumishi ambao ni viongozi wa kisiasa na menejimenti, hasa katika masuala ya kinidhamu, hali ambayo inaathiri ufanisi wa kazi.
 
“Kutokana na kasoro hizo na ili kuhakikisha kazi za kiutendaji haziingiliani na kuathiriwa na shughuli za kisiasa, Serikali imeamua kutoa mwongozo mpya kwa lengo la kurekebisha kasoro zilizojitokeza.
 
“Kwa msingi huo, Serikali imetoa utaratibu utakaozingatiwa na watumishi wote wa umma watakaogombea nafasi za uongozi wa kisiasa katika ngazi mbalimbali,” ilisema sehemu ya waraka huo.
Waraka huo unasema madhumuni yake ni kuweka mipaka ya nafasi ya mtumishi wa umma anapoamua kushiriki kwenye shughuli za kisiasa bila kuathiri utendaji wa shughuli za Serikali.
Maelekezo  ya  Serikali:
“Mtumishi wa umma atakayeamua kugombea ubunge wa viti maalumu aruhusiwe kufanya hivyo na baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kumtangaza kuwa mbunge, utumishi wake ukome na alipwe mafao yake,” ilisema sehemu ya waraka huo.
Waraka huo unasema mtumishi atakayeamua kugombea ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki, Bunge la Jamhuri ya Muunguno na udiwani watalazimika kuacha kazi na kulipwa mafao yao.
“Mtumishi wa umma anayeteuliwa na waziri mwenye dhamana ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuwa diwani, atakuwa na hiari ya kuchukua likizo bila malipo kwa kipindi chote cha wadhifa huo.”
Pia waraka huo umesema endapo mtumishi atashindwa katika uchaguzi na anataka kurudi kwenye utumishi wa umma, hana budi kuomba upya ajira kwa mamlaka zinazohusika.
Aidha waraka huo umeonya kuwa mtumishi atakayekiuka maelekezo hayo atachukuliwa hatua za kinidhamu, ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu katika chombo anachokisimamia.
Waraka huo umetolewa kwa mujibu wa kifungu cha 8 (1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 na kuanza kutumika Desemba mosi, 2014.
Masharti hayo ni tofauti na utaratibu uliokuwapo awali ambao unaruhusu mtumishi wa umma kugombea nafasi za kisiasa kwa kuomba likizo bila malipo, huku akitambuliwa bado ni mtumishi aliyepo kazini