Ushairi na Mashairi

Wakati mwingine umewahi kusikia watu wakisema au kuzungumzia “mashairi”. Utasikia wakisema daaah “jamaa ana mistari mikali“. Ukifuatilia kwa makini utakuta amepanga maneno yake katika maandishi ambayo yanaleta maana na ujumbe fulani wa kimaisha ambao hujenga hisia na ladha katika mpangilio huo na pale vinapowekwa vionjo vya mapigo ya kimuziki ndipo maana zaidi inaongezeka na kuwavutia watu wengi zaidi.

Katika ukurasa huu utapata kuona, kujifunza, kusikiliza na kutofautisha aina mbalimbali za mashairi na namna mtu anavyoweza kughani au kuimba mashairi hayo.

mashairi na ushairiMashairi ni nini?

Shairi ni kipande cha maandishi kilichopangwa kwa utaratibu katika mistari. Sauti za silabi hufanana zikiwa kati au mwisho mwa mstari. Maandishi hayo yakisomwa huleta ujumbe na hisia fulani ya kimaisha.

Mpango wa maneno ya shairi, ambao huweza kuimbwa hutoa picha wazi, maana halisi na burudani ya kimuziki. Nyimbo nyingi za makabila zimepangiliwa kishairi ijapokuwa hazikuandikwa.

Mashairi ya umbo ambalo huonekana kwa mpangilio wa sauti na idadi ya maneno katika mistari. Umbo hili hutofautisha shairi na tenzi.

kuna mambo kadhaa yanayotakiwa kufahamika kuhusu shairi, nayo ni;

 1. Beti – Kifungu kimoja cha shairi ambacho kina uzani sawa.
 2. Vina – Ni mwisho wa mistari ambayo huwa na silabi zenye sauti ileile mwishoni mwa sentensi.

Kuna vina vya kati na vya mwisho. Wakati mwingine huwa kuna vina vya mwanzo ambavyo huitwa bahari.

Mfano – Shaabani Robert, Pambo la Lugha uk. 9;

Upekwe faida yake, nimekaa nikiwaza,

Heri leo nitamke, haufai kutunza,

Upweke ni makeke, hasa siku za giza,

Itakapo watu wake, nchi kuiongoza.

katika beti hii moja, tunaona kuwa sentensi zina vina viwili – katikati (ke) na mwisho (ze)

3. Mizani – Ni idadi zilizo sawa za silabi katika kila mstari, ubeti hadi ubeti.

4. Kituo – Huu ni mstari wa mwisho wa ubeti.

kuna vituo vya aina tatu;

 • Kituo cha bahari – ni mstari unaotoka mwanzo hadi mwisho bila kubadilika katika kila ubeti.
 • Kituo cha kimalizio – ni kituo ambacho mstari wa mwisho maneno yake hubadilika ubeti hadi ubeti.
 • Kituo nusu bahari – ni mstari wa mwisho ambao maneno yake nusu hubadilika na nusu hubaki kama ulivyo ubeti hadi ubeti.

Katika mashairi, kila mstari lazima uwe umekamilika na ubeti uwe na maana kamili.

7 thoughts on “Ushairi na Mashairi

 1. sabilia ni shairi ambalo kibwagizo chake kina badililka badilika,je ikiwa ni hivyo basi hiyo haitakuwa kibwagizo kwani kibwagizo nadhani huwa haibadiliki.niweke sawa hapo bingwa.

  Like

 2. Nukuu ni nzuri zinaninufaisha sana, lakini naomba utuwekee nukuu za masomo yote pia na majibu ya mitihani ya kujipima ili tujipime kwa uhakika.

  Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.