SEHEMU A
- Nini maana ya Elimu ya Awali?
- Taja faida tatu azipatazo mtoto wa Elimu ya Awali anapojifunza kwa vitendo.
- Taja vigezo vinne (4) utavyotumia kuchagua mbinu za kufundishia E/awali.
- Taja malengo ya ufundishaji Elimu ya Awali.
- Eleza maana ya upimaji kwa mtoto wa Elimu ya Awali.
- Taja aina kuu za upimaji wa mtoto wa Elimu ya Awali.
- Kwa nini ni lazima kila mtoto aanzie madarasa ya E/Awali kabla ya kuanza darasa la kwanza?
- Taja misingi minne (4) ya ufundishaji E/Awali.
- Nini tofauti kati ya mbinu za maelezo na mbinu za vitendo.
SEHEMU B
10. Eleza jinsi mtoto wa Elimu ya Awali anavyopimwa ukilinganisha na mtoto wa shule za msingi.
11. Taja vitendo sita (6) mtoto wa Elimu ya Awali anavyopaswa kujifunza.
SEHEMU C
12. Nini maana ya maneno yafuatayo;
a. Kithembe b. Kigugumizi c. Akili taahira
13. Ufundishaji wa Elimu ya Awali ni tofauti na ule wa shule za msingi. Jadili.
14. Mwalimu wa Elimu ya Awali anapofundisha darasa lake anashauriwa kubadili tendo mara kwa mara. Jadili.
15. Katika shule ya msingi mwalimu anakazia ukimya wakati akifundisha. Lakini katika darasa la Awali mwalimu anaombwa asihangaishwe sana na mazungumzo ya watoto wakati wanapojifunza, kwa nini? Jadili.
Nafurahi sana jnsi ninavyo tembelea page hii nakupata mambo mengi nisiyo ya fahamu
LikeLike
Maswali mazuri hakika
LikeLike
Hakika haya maswali ni mazuri tena na tena nimefurahi kuyaona sinabudi kuyafuzu ili niwafundishe watotn wa elimu ya awali
LikeLike