Vifaa vya Mtaala

VIFAA VYA MTAALA

Mtaala una vifaa vyake maalumu ambavyo vinatakiwa vitumike kwa usahihi ili kutekeleza mtaala kwa ufaninsi. Vifaa hivyo ni;

 1. Muhtasari
 2. Vitabu vya kiada
 3. Kiongozi cha mwalimu
 4. Kitabu cha mwalimu na
 5. Rejea.

MATAYARISHO YA UFUNDISHAJI

Mtayarisho ya ufundishaji ni ile hali ya mwalimu kuandaa zana na vifaa muhimu kwa ajili ya kufundishia na kujifunzia

UMUHIMU WA MATAYARISHO YA UFUNDISHAJI

Kazi ya kufundisha ni kazi ya kitaalamu hivyo inahitaji maandalizi wakati wote. Hivyo basi mwalimu anapaswa kufanya maandalizi ya kutosha kabla ya kuingia darasani kufundisha na kwa mantiki hiyo mwalimu analazimika kujiandaa ili kuepuka matatizo yafuatayo wakati wa kufundisha na kujifunza.

 • Kukosa mtiririko unaofaa wa ufundisahaji
 • Kufundisha kwa kubahatisha au kubabaisha
 • Kuchosha wanafunzi katika kujifunza
 • Uwezekano wa kupotosha maudhui
 • Kushindwa kutunza muda
 • Kushindwa kukidhi matarajio ya somo na ya wanafunzi
 • Kujiamini au kutojiamini kusiko na misingi dhahiri

Kumbuka:

Ili Mwalimu aweze kukamilika katika maandalizi yake ya ufundishaji wa kila siku ni muhimu awe na baadhi ya vifaa ambavyo ndivyo msingi muhimu na muongozo muhimu wa kazi yake. Miongoni mwa vifaa hivyo ni;

 1. Muhtasari wa somo
 2. Azimio la Kazi
 3. Andalio la Somo
 4. Shajara la somo nk.

40 thoughts on “Vifaa vya Mtaala

  1. 1.msingi wa ufundishaji na ujifunzaji unaozingatia vitendo.
   2.msingi wa ufundishaji na ujifunzaji unaozingatia udadisi
   3.msingi unaozingatia usalama wa wanafunzi na vifaa vya tehama
   4.msingi unaozingatia urari wa jinsia na masuala mtambuko

   Like

 1. ni dhahali kabisa walimwakifuata vigezo vyote vya mtaala elimu ya tanzania inaongezeka kiwango cha ushindani wa kimataifa pia wanaohusika na uandaaji wa mtaala wasiwe wanabadilibadili mtaala.Vilevile vitabu vya kufundishia visibadilishwe mara kwa mara sababu kuepuka upotoshaji wa
  ufundishaji.

  Like

 2. Jamani vip kuhusu kitabucha kiada, kwenye vitu vinavyo fanya mwl aweze kukamilika ktk maandaliz yake ya ufundishaj wa kilasiku?

  Like

 3. Nisaidieni hayo maswal ndugu walimu
  1.Andika sababu za kutumia tathimn tamati katika kutathimn mtaala.
  2.Kwa kutoa mfano nn maana ya mkoba wa kazi?.

  Like

  1. Kitabu cha mwongozo ni kama mashine ya kuchakata somo katika vipengele vidogo vidogo na hukueleza uanze na nini.

   Like

 4. Kuna mkanganyiko wa maarifa ya iwspo mwalimu anaweza kuws zana au la. Nukuu nyingine inasema, mwalimu hawezi kuwa zana

  Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.