Azimio la Kazi

Azimio la Kazi ni nini?

Ni mwongozo unaoandaliwa na Mwalimu ambao unaonesha mpangilio wa kufundisha mada mbalimbali katika Muhtasari wa somo husika.

DSC00188Mwongozo huu unatokana na Muhtasari wa vitendo vya masomo (kwa elimu ya awali) au somo na uonesha mpangilio wa Mada Kuu na Mada Ndogo ambazo zitafundishwa darasani kwa muda uliopangwa.

Kwa ujumla Azimio la kazi ni mpangilio au utaratibu unaomwezesha mwalimu kuchanganua muhtasari wa somo na kupanga mada na jinsi atakavyozifundisha katika kipindi cha wiki, mwezi na muhula. Azimio la kazi huonesha njia atakazotumia mwalimu katika ufundishaji wake katika kila mada, na vifaa atakavyohitaji.

Hivyo, azimio la kazi ni mpango wa ufundishaji kwa kipindi fulani.

 

 

UMUHIMU WA AZIMIO LA KAZI

 • Kuandaa andalio la somo kunahitaji rejea ya azimio la kazi
 • Ufundishaji unahitaji kwenda na mtiririko mzuri wa mada
 • Kutoa nafasi ya kufanya marekebisho ya mwelekeo inapobidi
 • Huonesha wapi mwalimu alipofikia hivyo kumpa nafasi mwalimu anayempokea somo lake kujua pa kuanzia
 • Huonesha zana na vifaa vya kumsaidia mwalimu katika ufundishaji wake
 • Humuonesha mwalimu muda wa kufundisha kila mada
 • Huonesha malengo ya ufundishaji wa somo hilo katika muda aliopanga na jinsi alivyojitahidi kuendana na muda huo

VIPENGELE MUHIMU VYA AZIMIO LA KAZI

Muhula:

Sehemu hii huandikwa namba ya muhula ambapo azimio la kazi litatumika

Mwezi:

Huandikwa jina la mwezi ambapo mada fulani zitafundishwa

Ujuzi:

Ni maarifa, stadi na muelekeo anaoupata mwanafunzi baada ya kujifunza mada husika.

 • Maarifa, ni utambuzi anaoupata mtu au mwanafunzi baada ya kujifunza jambo fulani
 • Stadi, ni ule uwezo wa mwanafunzi kutumia viungo vyake vya mwili kufanya jambo linalotokana na somo alilojifunza, mfano kucheza, kuumba vitu mbalimbali, kufanya majaribio katika maabara, ufaraguzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia.
 • Mielekeo, inahusu mabadiliko yanayohusu stadi za maisha.Hii ni pamoja na mwanafunzi anavyobadili mwelekeowake kutokana na mambo aliyojifunza.

Wiki:

Sehemu hii huandikwa idadi ya wiki katika mwezi fulani ambapo sehemu fulani ya mada itafundishwa

Idadi ya vipindi:

Huandikwa idadi ya vipindi watakavyofundishwa katika idadi ya juma au majuma yaliyooneshwa

Mada kuu:

Hapa huandikwa mada kuu husika kama inavyoonekana katika muhtasari wa somo

Mada ndogo:

Hapa hujazwa mada ndogo kama ilivyo katika muhtasari wa somo

Vitendo vya ufundishaji:

Hapa hujazwa vitendo atakavyofanya mwalimu katika kujiandaa kufundisha mada husika na atakavyowashirikisha wanafunzi katika harakati za kufundisha na kujifunza

Vitendo vya ujifunzaji:

Hapa hujazwa vitendo vitakavyofanywa na wanafunzi kwa maelekezo ya mwalimu. Vitendo hivyo ama ni vya kujiandaa kujifunza katika muhula ufuatao au wakati uliopo wa muhula

Vifaa/zana:

Katika sehemu hii mwalimu anapaswa kuonesha vifaa au zana mbalimbali atakazotumia wakati waufundishajiwa mada ili kuweza kufanikisha ufundishaji na kuweza kufikia lengo lako mahsusi

Rejea:

Hapa mwalimu ataonesha vitabu alivyotumia kama rejea katika mada anayofundisha

Maoni:

Katika safu hii mwalimu atatoa maoni yake kuhusu mafanikio aliyoyaona, matatizo yaliyojitokeza na mapendekezo ya kuboresha ufundishaji.

Mfano wa Azimio la Kazi
Mfano wa Azimio la Kazi

 

48 thoughts on “Azimio la Kazi

   1. Nlikua naitaji ufafanuzi zaidi juu ya kipengele cha matayarisho ya ufundishaji ambapo kuna dhana ya matayarisho, azimio la kaz azimiio la somo, nukuu za somo, shajara la somo .na zaidi ahsanten km mtanisaidia

    Like

  1. Tunashukuru kwa ufafanuzi muda si mrefu tutaweka nukuu nzuri zenye mifano za Azimio la Kazi, Andalio la somo na zingine nzuri jisajili kwenye “Follow us” ili kila tuwekapo nukuu mbalimbali uwe unapata taarifa moja kwa moja….tunakutakia masomo mema

   Like

 1. Asnteni sana kwa kazi nzuri mnayoifanya lakini nomba kuuliza mnasemaje kuhusu masomo ya elimu ya awali yaani kuandaa notes/moduli zake na namna ya ufundishaji wake?

  Like

  1. Tunashukuru ngugu Joseph, kwa sasa bado tunaangalia namna mfumo mpya unavyokwenda ila kuanzia j3 tutawaletea namna gani ufanye ili uweze kukabiliana na ufundishaji wa Elimu ya Awali…..tembelea hapa mara kwa mara kwa maarifa zaidi na tunakutakia masomo mema

   Like

 2. Kweli inasemekana kuwa andalio la somo na azimio la kazi ni mwongozo katika ufundishaji, lakini vipi mbona katika baadhi ya shule za english medium ninazozijua katika ufundishaji wao wa darasa la saba inakuwa tofauti, haya mambo hayatumiki na ndo shule ambazo zinafanya vizuri kitaifa, kati ya shule hizo ndo unakuta zinakuwa za kwanza, pili tatu au nne. Je, kuna umuhimu kweli?

  Like

 3. mi ningeshauli na wafanyakaz wengine maofisin wawe na maazimia yao, naamin nchi itapiga maendeleo ya haraka na big result now tungeiona ktk sector zote…ahsante

  Like

  1. These explanations concerning the components of scheme of work it has kunaring my heart, I mean that it has impressed me because it is very easy to understand, may God bless you thanks much.

   Like

 4. Maelekezo yako kuhusu uandaaji wa azimio la kazi ni mazuri lakini Nigeria mfano HAMISI japo kwa wiki moja ili mwalimu tarajali ajifunze lugha ya kuandika hasa katika kipengele cha VITENDO VYA MWALIMU na VITENDO VYA MWANAFUNZI!

  Like

  1. Maelekezo yako ni mazuri kuhusu uandaaji wa azimio la kazi lakini ingekuwa vizuri zaidi kama ungetoa mfano halisi japo kwa wiki moja ili walimu tarajali wajifunze lugha itumikayo hasa katika kipengele cha VITENDO VYA MWALIMU na VITENDO VYA MWANAFUNZI

   Like

 5. nimezifurahia sana mpangirio wakazi mlio uweka, pia nimezipenda sana notis zenu ni nzur mwenyezi awajalie katika mwendelezo wenu wa kuitatangaza elimu.thanx

  Like

 6. nashukuru sana ila sijajua azimio jipya lipoje? na nikitaka kuingia (log in) kwa kutumia e mail angu na password nakataliwa sijajua tatizo nini ktk website yenu nashindwa

  Like

 7. Huu mwongozo umenisaidia sana katika kujifunza kuandaa azimio la kazi katika tendo zima la kufundishia na kujifunzia kwa darasa husika na mada husika

  Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.