Kiongozi cha Mwalimu

KIONGOZI CHA MWALIMU

Kiongozi cha mwalimu ni kitabu kinachompa mwalimu maelekezo ya mada ya kufundisha, jinsi ya kufundisha, maudhui gani yafundishwe na kwa kutumia vifaa au zana gani.

Sifa za Kiongozi cha Mwalimu

Kitabu hiki kina mambo yafuatayo;

 • Utangulizi unaolekeza mambo makuu na muhimu yatakayozingatiwa katika ufundishaji. Utangulizi huo pia utaelekeza mgawanyo wa muda unaofaa katika kufundishia mada mbalimbali
 • Malengo mahsusi ya kufundisha kila mada
 • Mapendekezo ya njia na mbinu za kufundishia na kujifunzia
 • Mapendekezo ya vifaa na zana zinazofaa kufundishia kila mada
 • Mazoezi yanayolingana na mada zilizo katika kitabu cha kiada
 • Jinsi ya kupima ujifunzaji wa wanafunzi
 • Mapendekezo ya vitabu vya rejea vitakavyosaidia kutoa maarifa
 • Majibu  ya maswaliyaliyomo katika kitabu cha kiada

Matumizi ya Kiongozi cha Mwalimu

 • Kitabu hiki hutumika sambamba na kitabu cha kiada
 • Hutumiwa na mwalimu kuandaa masomo na zana
 • Pia hutumika kuandaa mazoezi ya nyongeza kwa wanafunzi

Umuhimu wa Kiongozi cha Mwalimu

 • Kumwelekeza mwalimu jambo la kufanya, hivyo humpa dira au mwelekeo wa ufundishaji
 • Humsaidia mwalimu kujijengea moyo wa kujiamini na hasa kama si mzoefu wa ufundishaji wa somo hilo
 • Humsaidia mwalimu katika kuandaa somo
 • Humpa mwalimu maudhui na mifano ya ziada kuzidi kumpanua mawazo na upeo

7 thoughts on “Kiongozi cha Mwalimu

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.