Kitabu cha Kiada

Dhana ya Kitabu cha Kiada

Kitabu cha kiada ni kile kinachofafanua mada zote za muhtasari kwa ukamilifu. Kitabu hiki ndicho kinachobeba maudhui ya somo kwa ukamilifu.

Sifa za Kitabu cha Kiada

Kitabu cha kiada hutumiwa na mwalimu pamoja na mwanafunzi kwa hiyo kinatakiwa;

 • Kiwe chenye lugha rahisi inayoeleweka kulingana na kiwango cha mwanafunzi
 • Kiwe na mada zilizopangwa kwa mtiririko wenye mantiki kuanzia mada rahisi hadi zile  ngumu
 • Kiwe na maandishi yanayosomeka kwa urahisi na ya kuvutia. Mpangilio wake uwe wa kuvutia kiwe na picha pamoja na vielelezo ili kumvutia mwanafunzi na kurahisisha usomaji
 • Kiwe na jalada gumu, thabiti na linalovutia
 • Kisiwe kinene sana
 • Kiwe na maelakezo na mazoezi yanayomshirikisha mwanafunzi katika kujifunza
 • Kiwe kinaendana na muhtasari pamoja na kiongozi cha mwalimu

Matumizi ya Kitabu cha Kiada

 • Hutumiwa na mwanafunzi kwa kujisomea na kupata maarifa na maelekezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mazoezi
 • Mwanafunzi hukitumia katika kujikumbusha na kufanya marudio katika kujiandaa kwa mitihani
 • Hutumiwa na mwalimu kuelekeza maarifa, matendo na mazoezi mbalimbali kwa mwanafunzi kwa kutumia picha, maudhui, ramani na vielelezo vingine vilivyo kitabuni

Uchambuzi wa Kitabu cha Kiada

Vitabu mbalimbali vya kiada vimeandikwa kwa mitindo tofauti tofauti. Kwa utaratibu wa sasa wa biashara huria ya vitabu, somo moja huweza kuwa na vitabu kadhaa. Ni jukumu la mwalimu wa somo pengine kwa kushirikiana na wanafunzi wake kuwa makini katika kuchagua kitabu kinachofaa zaidi.

3 thoughts on “Kitabu cha Kiada

 1. Mawazo mazuri sana.
  Kitaaluma vitabu vingi vlivyo na miundo mbalimbali vinachanganya watu, hii ni kutokana waandishi kutokufanya uchunguzi na utafiti wa kutosha.

  Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.