Kitabu cha Mwalimu

KITABU CHA MWALIMU

Kitabu cha mwalimu ni kitabu kinachotoa maelekezo ya kina kuhusu ufundishaji wa somo fulani. Kinaelekeza jinsi ya kutenda katika hatua zote tangu uandaaji wa somo, ufundishaji hadi upimaji. Ni muongozo unaompa mwalimu ujuzi wa kiufundishaji.

Sifa za Kitabu cha Mwalimu

 • Kina vitendo vyote ambavyo mwalimu hupaswa kuvitenda katika hatua za kufundisha
 • Kinaelekeza jinsi ya kutekeleza kazi ya ufundishaji hatua kwa hatua
 • Kinatoa ufafanuzi wa mada katika kiwango cha juu zaidi ili kupanua mawazo ya mwalimu na kumuimarisha zaidi katika eneo hilo la taaluma
 • Huweza kutumiwa na mwanafunzi pia

        Tofauti kati ya Kitabu cha Mwalimu na Kiongozi cha Mwalimu

 tofauti

Umuhimu wa Kitabu cha Mwalimu

 • Humwezesha mwalimu kufuata maelekezo hatua kwa hatua ili kukamilisha kwa njia inayofanana
 • Hurahisisha tathmini
 • Husaidia walimu ambao si wazoefu wa kazi

MAANDIKO YA REJEA

Hakuna kitabu wala maandiko yoyote ya kitaaluma ambayo hujitosheleza kikamilifu katika kueleza mada fulani. Hii ni kwa sababu wataalamu wapo wengi na pia wanatofautiana katika kuandika. Rejea si lazima iwe kitabu, bali hata makala, magazeti, majarida, vitini ambavyo hutumiwa na mtu anapohitaji kupata taarifa au maarifa maalumu.

SIFA ZA MAANDIKO YA REJEA

 1. Maandiko ya rejea yawe na maudhui au vielelezo vinavyohusiana au kufanana na maudhui ya muhtasari na kitabu cha kiada cha somo husika
 2. Hakina ulazima wa kuwa na mada zote zilizo kwenye muhtasari wa somo husika

Umuhimu wa Maandiko ya Rejea

 1. Maandiko ya rejea humuongezea msomaji maarifa na ujuzi kuhusu jambo fulani
 2. Humwondolea muhusika wasiwasi, mkanganyiko au utata ambao inawezekana ameupata kutokana na vyanzo vya habari
 3. Rejea humuongezea msomaji ari ya kusoma zaidi ili kuelewa jambo kwa undani
 4. Humpa mwanfunzi uhuru wa kujichagulia rejea za aina nyingi iwezekanavyo, hivyo hujenga moyo wa kujiamini zaidi
 5. Huongeza moyo wa ushindani katika kutafuta maarifa

2 thoughts on “Kitabu cha Mwalimu

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.