Muhtasari wa Somo

Dhana ya Muhtasari

Muhtasari ni mwongozo unaotaja kwa kifupi tu mambo yote yanayotakiwa yafundishwe katika mwaka mzima, katika darasa fulani au kwa miaka kadhaa kwa kila darasa kwa mpanglio maalumu. Muhtasari unaonyesha kitu gani kifundishwe kwenye somo, lini, kwa nani na kwa njia na mbinu zipi.

Muundo wa Muhtasari

Muhtasari una sehemu kuu mbili. Sehemu ya kwanza ni utangulizi, sehemu hii kazi yake ni kuelekeza sababu za kuwepo kwa muhtasari huo, muundo wake, malengo ya elimu katika kiwango husika na malengo ya kufundisha somo hilo katika kiwango hicho. Sehemu ya pili ni majedwali ya kutumia kufundishia. Ndani ya majedwali kuna maudhui ya somo hilo yanayotakiwa kufundishwa kila mwaka.

Vipengele vya Muhtasari

  1. Mada kuu na mada ndogo
  2. Lengo la kufundisha mada hiyo
  3. Njia za kufundishia na kujifunzia
  4. Vifaa au zana za kufundishia na kujifunzia

Matumizi ya Muhtasari

Muhtasari ndio mwongozo mkuu wa mwalimu wa kufundisha somo katika darasa lolote.

Matumizi

  • Kumwongoza mwalimu kuandaa maazimio ya kazi na maandalio ya masomo
  • Kuongoza waandishi wa vitabu vya kiada, kiongozi cha mwalimu na vitabu vya rejea
  • Kuelekeza njia zinazofaa katika kufundishia na kujifunzia
  • Kuandalia mwongozo wa upimaji wa maendeleo ya wanafunzi kwa mwaka au kwa kipindi cha miaka kadhaa
  • Kutathmini mtaala baada ya kipindi maalumu cha matumizi ya muhtasari huo

13 thoughts on “Muhtasari wa Somo

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.