KUMBUKUMBU ZA SOMO
Shajara/Kumbukumbu za somo (logbook) ni muhtasari unaotayarishwa na mwalimu wa somo kuonesha mada kuu na mada ndogo alizofundisha, wakati (lini) alipofundisha na jina au sahihi yake.
Pamoja na kumbukumbu hii mwalimu ana kumbukumbu zingine ambazo zinatumika kama rejea za kazi alizofanya mfano azimio la kazi, andalio la somo pamoja na nukuu za somo.
UMUHIMU WA KUMBUKUMBU ZA SOMO
Mwalimu anatakiwa kutunza kumbukumbu za somo analofundisha.kumbukumbu za somo ni muhimu kwa sababu:
- Huonesha bayana mambo yaliyofundishwa na wakati yalipofundishwa
- Humwelekeza mwalimu mpya mahali pa kuanzia
- Mwalimu huweza kupima kiasi cha mada alizokwisha fundisha kwa kulinganisha na azimio la kazi
- Huonesha kazi zilizofanywa na mwalimu aliyeondoka
- Huweza kutumika kutathmini kasi ya ufundishaji wa mada
I like this #page.
LikeLike
JE NILAZIMA MWALIMU AANDAE ANDALIO LA SOMO KILA SIKU AINGIAPO DARASANI
LikeLike
Usikae kimya na sio (Usikae kimia…..) kama ulivyo andika.🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌…nukuu nzuri.
LikeLike
Nukuu nzuri sana asante
LikeLike
mbona huo mchoro haukufuata muhamo wa ruwaza
LikeLike
Za uong
LikeLike