Zana za Kufundishia

Kazi ya kufundisha haina zana maalumu kama kazi nyingine. Zana zozote zinaweza kutumika katika kazi ya kufundisha. Zana za kazi hii zinapata jina lake wakati zinapotumiwa na Mwalimu au Mwanafunzi katika kufanikisha tendo la kufundisha na tendo la kujifunza.

Huwezi kuviita visoda au ramani zana za kujifunzia/kufundishia isipokuwa vinapotumiwa na Mwalimu au Mwanafunzi. Kiwango cha elimu katika shule zetu kitapanda zaidi ikiwa walimu watafanya juhudi katika kutayarsisha, kutengeneza na kutumia vema zana za kufundishia/kujifunzia zilizo muafaka kwa somo linalohusika, kuwa na moyo, ari, juhudi na mwelekeo mzuri wa kufanikisha kazi yao kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu nchini.

Lakini mambo sivyo yalivyo katika shule zetu. Imekuwa ni jambo la kawaida kwa walimu kuwa na tabia ya kukwepa kutumia zana za kufundishia/kujifunzia ingawa zana zinapatikana shuleni. Mwalimu kumbuka usemi unaosema “Kuona ni kuamini“, wanafunzi watakuamini na wataamini somo ikiwa watakiona wanachojifunza.

Walimu wanajenga dhana ya kuwa kufundisha ni kuhubiri kwa kutumia mdomo na chaki peke yake. Dhana hii ni potofu na inachangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa kiwango cha elimu nchini.

Kumbuka “Mti hauendi ila kwa nyenzo“, huu ni usemi maarufu wa kiswahili ambao umeficha maana na falsafa ya maisha yetu ya  kila siku. Kazi yoyote inakuwa rahisi, yenye ufanisi na yenye kutoa matunda bora iwapo itapata vitendea kazi sahihi.

12 thoughts on “Zana za Kufundishia

 1. kaka Gunda, vifaa vya kufunzia ndicho kiungo cha wanafunzi na mwalimu katika mhadhara au somo lolote lile. Uliyoyasema hapo juu kuhusu suala hili ni ekweli mtupu unaohitaji walimu wote kuuenzi na kuutumia ili kufanikisha mchakoto huu wa ufundishaji na ujifunzaji. Hongera.

  Like

  1. Nashukuru sana Mwalimu Iyaya, tupo pamoja, pia ni wajibu wetu kuinua taaluma ya elimu nchini na ni jukumu letu sote, nashukuru kwa kuliona hilo na hata wewe tunakukaribisha kwa makala yeyote ya kielimu uliyonayo tyutaiweka humu na jamii yetu waisome..karibu sana

   Like

 2. Hongera sana hebu sasa wapatie walimu umhimu wa kutumia zana na madhara ya kutotumia zana katika tendo zima la kufundisha na kujifunza darasani

  Like

 3. Zana ni muhimu xana katika zoez la ufundishaji na ujifunzaji coz humfanya mwanafunzi aone vifani/vitu halisi anavyojifunza.

  Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.