Zana za Kujifunzia na Kufundishia

Mwalimu yeyote anapaswa kujifunza utengenezaji na matumizi ya zana, kwani ni nyenzo muhimu sana katika kazi ya kufundisha na kujifunza.

Nini maana ya Zana za Kujifunzia na Kufundishia?

“Zana ni kitu chochote kinachopangwa na kutumika katika kuinua kiwango cha elimu”.

Je, mwalimu anaweza kuwa Zana?

NDIYO,  Mwalimu pamoja na vifaa vingine anaweza kuwa zana kwa sababu vifaa vya kufundishia pamoja na mwalimu vimepangwa na kutayarishwa kwa madhumuni ya kuboresha tendo la kujifunza na kufundisha.

Je, unadhani Mwanafunzi anaweza kujifunza pasi kuwa na Mwalimu?

NDIYO, Mwanafunzi anaweza kujifunza kwa kutumia zana pekee bila ya mwalimu (Resource-based learning) lakini mwalimu atashindwa kufundisha bila ya mwanafunzi ingawa anazo zana za kufundishia.

JIPIME

Mwalimu anaposimama mbele ya darasa na zana zake, Je, madhumuni na lengo lake ni kuinua kiwango cha wanafunzi kujifunza au kuinua kiwango chake cha kufundisha?

KUMBUKA

Lengo hasa la kutumia zana katika kufundisha ni kukuza na kuinua kiwango cha kujifunza cha mwanafunzi.

Aina mbalimbali za Zana za Kujifunzia na Kufundishia

Piramidi la Zana
Piramidi la Zana

Zana za Kufundishia na Kujifunzia zimegawanyika katika makundi matano (5);

 • Vitu Halisi

Kutokana na mpangilio wa piramidi, vitu halisi ni bora zaidi kwa Kufundishia kuliko kifaa cha aina nyingine ile.

Kwa kutumia vitu halisi mwanafunzi anajifunza kwa udadisi, kuchunguza, na kugundua. Pia vitu halisi vinampa mwanafunzi nafasi kubwa ya kujifunza kwa vitendo na kutumia milango mingi ya fahamu kwa wakati mmoja. Katika Piramidi vitu halisi vimewekwa kwenye kitako cha piramidi kuonesha umuhimu wa utumiaji wa vitu halisi wakati wa kujifunza na kufundisha.

 • Bandia/Maumbo (Model)

Kwa ukosefu wa vitu halisi, maumbo/vitu bandia huchukua nafasi ya pili. Mwanafunzi anapata kuona, kusikia, kuhisi kana kwamba anatunmia vitu halisi. Bandia ni igizo la vitu halisi, hivyo huchangia iasi Fulani cha ukweli.

 • Televisheni, Video na Sinema

Televisheni inachangia katika kuonesha vitu kama vilivyo, kwa hali hii kuna ukweli ndani ya televisheni. Televisheni inamwezesha mwanafunzi kusikia na kuona matendo wakati ule ule yanapofanyika.

 • Chati, Picha, Mabango, Grafu na Ramani

Zana hizi hutoa mawasiliano ya kuona tu. Mwanafunzi anajifunza kwa kutumia macho yake tu.

 • Radio, Santuri, Tepu-Rekoda

Zana hizi humsaidia mwanafunzi kujifunza kwa kusikia. Vipindi maalum hutayarishwa kwa ajili ya shule au wanafunzi wanaosoma kwa masafa.

JIPIME

Toa sababu ya mpangilio wa zana za kujifunzia na kufundishia kupangwa kwa umbo la piramidi.

Mgawanyo wa Zana za Kujifunzia na Kufundishia

Zana za Kujifunzia na Kufundishia zinaweza kugawanywa katika makundi makuu mawili (2);

Zana za Ziada

Hizi ni aina ya zana zinazomsaidia mwalimu kuchapuza somo lake. Kwa kutumia zana za ziada mwanafunzi hapati fursa ya kujifunza kwa vitendo yale mambo anayojifunza, bali mwanafunzi hubaki kusikiliza tu. (mfano radio, tepu rekoda na santuri).

Zana Unganishi

Hizi ni aina ya zana zenye msaada mkubwa wakati wa ufundishaji. Zanan unganishi hazimsaidii mwanafunzi katika kujifunza tu bali zinamsaidia mwanafunzi kufanya kwa vitendo yale anayojifunza.

(mfano vitu halisi, bandia, chati, ramani, picha, na maabara)

57 thoughts on “Zana za Kujifunzia na Kufundishia

  1. Zana ni za aina mbili asili na kisasa. Yapo makundi makuu matatu, nayo ni zana maono, masikizi na masikizi_maono

   Mtaala rasmi na usio rasmi.

   Like

 1. nilikuwa sijaiona hii am kweli mwalimu Gunda kuanzia sasa ntakuwa nakufatilia sana isiyoshe mimi nachukua au nasomea ualimu elimu ya awali hivyo najua utanisaidia sana,mungu na akubariki sana lakii nakuomba sana ukiwa na chochote nitumie basi kwenye email yangu at jraphael671@gmail.com

  Liked by 1 person

 2. Kwanza napenda kuwapongeza kwa huduma yenu hii,mnatusaidia sana wanachuo kwa kias kikubwa…ningependa kujua kama naweza kuongeza”zana mguso” ktk makund ya zana.

  Like

 3. Ninashukuru kwa maelezo juu ya aina za zana lakini bado natatizika kwani nilipokuwa chuo cha ualimu nilisoma moduli nikabaini makundi matatu ya zana ambazo ni zana maono/za kuonekana mf. beseni, zana masikizi/za kusikika mf. redio na zana maono-masikizi mf. runinga.Wengine wanasema kuwa kuna zana halisi na zana bandia, Je kundi lipi ndio sahihi au au aina za zana zinabadilika kulingana na kiwango cha elimu? kwani mwanafunzi wa darasa la 1 anaambiwa kuwa 0-2 haiwezekani lakini akifika darasa la 5 huambiwa kuwa inawezekana.Naomba maelezo ya kina ili nijue usahihi wa jambo hili.

  Like

 4. Nashukuru kwa msaada wenu maana mmetusaidia sana ss walimu ila bado napata utata kuhusu makundi ya zana sababu nikisoma kwenye moduli naambiwa yapo makundi matatu.

  Like

 5. Nashkuru sana kwa kunisaidia na maelezo kuhusa makundi mawili ya zanb za kufundishia kufanya mjarabu wangu. asanteni sana

  Like

 6. Mimi najua kuwa zipo aina tatu za zana,ambazo ni zana za kuona,zana za kusikika na zana za kuona na kusikika.Je!kuna mabadiliko yaliyojitokeza hivi karibuni? Naomba kusaidiwa.

  Like

 7. Nimependa moyowenu wa huduma.mafunzo yenu na utafiti wenu kwa uelewa wa wanafunzi wetu na maendeleo kwaujumla.

  Like

 8. Nimefurahishwa sana taarifa hii maana nilikuwa sijui kama Luna piramidi ya zana naomba endelea kutusaidià maana semina za elimu kwa mwalimu mmoja mmoja Hanna kutokana na serikali kutokuwa nahela

  Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.